Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA

Askari waendelea kukamatwa nchini Burundi

Jeshi la Burundi linaendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu, huku idadi ya askari wanaoendelea kukamatwa ikiendelea kuongezeka kila kukicha. Hali hii ilianza kushuhudiwa toka Jumanne wiki hii.

Askari waendelea kukamatwa katika kambi mbalimbali nchini Burundi.
Askari waendelea kukamatwa katika kambi mbalimbali nchini Burundi. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Tukio la mwisho ni la afisa wa cheo cha Meja na mwengine wa cheo cha Luteni wa kambi ya mkoa wa Muyinga waliokamatwa hivi karibuni baada ya kusikika milio ya risasi karibu na kambi hiyo ya jeshi mashariki mwa Burundi.

Awali kesi hii ilionekana kuwa dogo, lakini tangu wakati huo askari wengi wamekamatwa na tayari hali imeanza kutisha.Milio ya risasi ilisikika karibu ya kambi ya jeshi ya Mukoni mkoani Muyinga usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii.

Wakazi wa eneo lililo karibu ya kambi wanahakikisha kwamba kambi hii ya jeshi ilikuwa ililengwa na mashambulizi ya waasi. Madai ambayo yamekanushwa na msemaji wa jeshi, ambaye amesema ilikua tu wezi wa kawaida ambao walirusha risasi hewani wakati walipowaona askari wakipiga doria karibu na kambi hiyo. Lakini silaha ziliokotwa karibu na kambi hiyo.

Baada ya tukio hilo, afisa wa jeshi katika kambi hiyo ya Mukoni alikamtwa siku ya Jumanne mchana. Baadaye alitaja majina ya askari kutoka kambi zingine nchini walioshirikiana naye katika kitendo, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Burundi.

Kisha askari wa pili, François Nkunzimana, alikamatwa na raia kukabidhiwa polisi, kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi. Lakini mwili wake ulikutwa siku ya pili katika msitu mdogo ulio karibu na kambi huku ukiwa na majeraha ya risasi. Mwili wa askari huyo ulikua karibu ya miili mingine ya watu waliouawa kwa risasi. Wakati huo viongozi tawala katika wilaya ya Mukoni walitoa amri ya miili hiyo kuzikwa katika msitu huo

Tangu wakati huo, askari wameendelea kukamatwa katika makambi kadhaa ya jeshi ikiwani pamoja na mkoani Ngozi kaskazini mwa Burundi, mkoani Gitega katikati mwa nchi, na katika kambi ya Mutukura kaskazini mashariki mwa nchi. Kwa uchache askari 18 askari wamekamatwa, ikiwa ni pamoja na maafisa wawili.

Msemaji wa jeshi Kanali Gaspard Bratuza anatambua kwamba silaha zilibiwa katika kambi ya Mukoni Jumanne Januari 24. Baadhi ya maafisa wa jeshi wanabaini kwamba hali hii ya kamta kamata huenda ikazua hali ya sintofahamu katika jeshi kwa sababu wanaokamatwa ni askari waliokua wa jeshi la zamani la Burundi (ex-FAB) kabla ya kuingizwa katika jeshi wapiganaji wa zamani kutoka makundi mbalimbali ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.