Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA

Mauaji ya waziri wa mazingira: Watu watatu wakamatawa

Polisi ya Burundi imesema kuwa imewakamata watu watatu ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja ambao inawashtumu kuhusika katika mauaji ya Waziri wa Maji na Mazingira Emmanuel Niyonkuru.

Polisi ikipiga doria katika moja ya mitaa ya mjini Bujumbura, Aprili 12, 2016.
Polisi ikipiga doria katika moja ya mitaa ya mjini Bujumbura, Aprili 12, 2016. STRINGER / cds / AFP
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Maji na Mazingira Emmanue Niyonkuru aliuawa usiku wa kuamkia Jumapili Januari 1, 2017 alipokua akiingia kwa gari nyumbani kwake katika kata ya Rohero katikati mwa mji wa Bujumbura, kwa mujibu wa polisi, huku ikiongeza kuwa aliyetekeleza mauaji hayo hajulikani aliko.

Manispa ya jiji la Bujumbura inabaini kwamba mauaji ya Waziri Emmanuel Niyonkuru yaliendeshwa saa saba usiku za Afrika ya Kati.

Inaarifiwa kuwa Waziri Niyonkuru aliuawa kwa bastola.

Msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa polisi inamshikilia mwanamke aliyekua akiambatana na Waziri Niyonkuru kwa ajili ya uchunguzi.

Mapema asubuhi siku ya Jumapili, Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter : “Waziri Emmanuel Niyonkuru ameuawa usiku wa kuamkia leo. Rambi rambi zangu kwa familia yake na wananchi wa Burundi. Wahusika watahukumiwa kwa mujibu wa sheria.”

Itafahamika kwamba Mshauri Mkuu wa rais Pierre Nkurunziza Willy Nyamitwe aliponea kuuawa baada ya mlinzi wake kuuawa kwa risasi alipokua akirejea nyumbani kwake katika kata ya Kajaga kilomita 6 na mji wa Bujumbura mwezi mmoja uliyopita.

Mauaji nchini Burundi yamekithiri, watu wamekua wakipotezwa na baadaye wanaokotwa maiti na wengine kupelekwa sehemu zisizojulikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.