Pata taarifa kuu
UN-SUDAN KUSINI

Umoja wa Mataifa watishia kuiwekea vikwazo Sudan Kusini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaitaka Sudan Kusini kuchukua hatua ya haraka na kukubali jeshi la kulinda amani kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki, kuwasili jijini Juba la sivyo, iwekewe vikwazo vya kununua silaha.

Vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini
Vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini freedom.com
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa New Zealand Gerard van Bohemen, ambaye ni rais wa Baraza hilo kwa mwezi wa Septemba, amesema ni wakati wa serikali ya Juba kuchukua hatua.

Amesisitiza kuwa huu ni wakati wa rais Salva Kiir kuonesha kwa vitendo utekelezwaji wa hatua hii na kuacha kutumia maneno.

Mwezi uliopita, Baraza hilo lilipiga kura ya kutuma kikosi cha wanajeshi 4000 jijini Juba, kuhakikisha kuwa vita havishuhudiwi tena katika jiji hilo  lakini pia kulinda mali za Umoja wa Mataifa.

Wiki mbili zilizopita, wajumbe wa Baraza hilo walizuru jijini Juba kukutana na serikali ya Juba, wanasiasa wa upinzani na wanaharakati kuthathmini hali ya kisiasa na siasa nchini humo na kusisitiza umuhimu wa kuja kwa kikosi hicho.

Rais Salva Kiir ameonekana kutoliamini jeshi hilo la Umoja wa Mataifa, baada ya kudai kuwa linamuunga mkono mpinzani wake Riek Machar.

Mkuu wa vikosi vya kulinda amani katika Umoja wa Mataifa Herve Ladsous amesema rais Kiir hajaonesha nia ya dhati ya kukubali kutumwa kwa jeshi hilo licha ya kutoa hakikisho la kukikubali kikosi hicho wiki moja iliyopita.

Mataifa yatakayotoa kikosi hicho ni pamoja na Kenya, Ethiopia na Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.