Pata taarifa kuu
ZANZIBAR

Idadi ya miili ya watu waliokufa Zanzibar yafikia 89

Vikosi vya uokoaji visiwani Zanzibar nchini Tanzania vimefanikiwa kupata miili mingine kumi na moja kwenye aneo la tukio ambako meli ya Mv Skagit ilizama juma moja lililopita ikiwa na watu 290 na kufanya idadi ya watu waliokufa kufikia 89. 

RFI
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeendelea na juhudi za kusaka miili zaidi ambapo miili inayoendelea kupatikana inazikwa moja kwa moja kwenye makaburi ya halaiki kwakuwa imeshaharibika sana na sio rahisi kutambulika.

Inspekta Mohamed Muhina ni afisa habari mkuu wa jeshi la polisi huko visiwani Zanzibar na amethibitisha taarifa hizo huku akisema kuwa operesheni hiyo ya kusaka miili mpaka itakapoonekana hakuna uwezekano wa kupata miili zaidi.

Hapo jana serikali ya Zanzibar ilitangaza kusitisha safari za meli ya MV Kalama ambayo inamilikiwa na kampuni moja iliyokuwa ikimiliki meli ya MV Skagit baada ya kubaini kuwa ina mapungufu na haiwezi kufanya safari zake za Zanzibar na Dar es salaam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.