Pata taarifa kuu

DRC: Jean -Jacques Mamba ajiunga na vuguvugu la waasi la Alliance Fleuve Congo

Nairobi – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kujiunga kwa mbunge wa zamani Jean -Jacques Mamba katika vuguvugu la waasi la AFC linaloongozwa na rais wa zamani wa tume ya uchaguzi (CENI), Corneille Nangaa anaeshirikiana na waasi wa M23 imewashangaza wengi.

CIA world factbook
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Kinshasa haijasema lolote licha ya kupokea kwa mtazamo hasi sana, bali chama cha MLC ambacho mbunge huyo Jean Jacques Mamba alikuwa mwanachama ndicho kimetoa taarifa kueleza kuwa mbunge huyo wa zamani alijiuzulu mapema sana na hakuwa tena mwanachama.

Baada ya tangazo lake hapo jana Jumatatu akiwa  jijini Brussels  Jean Jacques Mamba la kujiunga na Muungano wa Alliance fleuve Congo (AFC), mamlaka mjini Kinshasa inajiandaa kuonyesa kukasirishwa kwake dhidi ya Ubelgiji.  Balozi wa Ubelgiji aliyeko Kinshasa anatarajiwa kuitwa na mamlaka kwa maelezo.

Kinshasa pia itamwita balozi wake mjini Brussels kwa mashauriano, kulingana na vyanzo mbalimbali vya habari. Maamuzi haya yajayo yanaweza kuelezewa na uhusiano wa kirafiki na historia ya pamoja iliyopo kati ya DRC na Ubelgiji,

Baada ya kutangazwa rasmi kwa kundi la AFC  Disemba 15 jijini Nairobi, Kinshasa ilimwita balozi wa Kenya aliyeko Kinshasa kabla ya kumwita mwakilishi wake aliyeidhinishwa jijini Nairobi kama ishara ya kupinga

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.