Pata taarifa kuu

Ugonjwa unaoathiri macho waripotiwa pwani ya Kenya

Nairobi – Wataalam wa afya nchini Kenya wanachunguza mlipuko wa maambukizo ya ugonjwa wa macho mekundu “Red eyes”, unaowasumabua wakaazi wa jiji la Mombasa na Kilifi pwani ya nchi hiyo. 

Wakaazi wa pwani ya Kenya wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizo hayo ya macho
Wakaazi wa pwani ya Kenya wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizo hayo ya macho © wikipedia
Matangazo ya kibiashara

 

Wakazi wameshauriwa kuzingatia kanuni za usafi kama vile kunawa mikono, kuepuka kushiriki vitu vya kibinafsi na kuacha kugusa macho yao. 

Wiki iliyopita, mamlaka za afya nchini Tanzania zilitoa tahadhari baada ya kurekodi visa 869 vya ugonjwa huo katika mwezi mmoja, wengi wao wakiwa katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam. 

Conjunctivitis, pia inajulikana kama ugonjwa mwekundu wa jicho ambapo pia unaifanya sehemu inayolinda macho kuvimba . 

Ugonjwa husababishwa na mzio au maambukizi na dalili zake ni  kama vile macho kuwa mekundu, uvimbe, machozi au kuwasha.  

Wagonjwa wengine wanaweza pia kutoa uchafu kutoka kwa jicho kwa mujibu wa maofisa wa afya. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.