Pata taarifa kuu

Kenya: Raia wa Nigeria wanazuiliwa kwa kuhusishwa na mauaji ya mwanafunzi

Nairobi – Polisi nchini Kenya inawazuilia wanaume wawili ambao inasema ni raia wa Nigeria wakihusishwa na mauaji ya mwanafunzi wa kike kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Mauaji hayo yamekuwa ya hivi punde kukashifiwa, wito ukitolewa kwa maofisa wa polisi kuanzisha uchunguzi zaidi kuwakamata wahusika na mauaji hayo ya kinyama
Mauaji hayo yamekuwa ya hivi punde kukashifiwa, wito ukitolewa kwa maofisa wa polisi kuanzisha uchunguzi zaidi kuwakamata wahusika na mauaji hayo ya kinyama Google map
Matangazo ya kibiashara

Licha ya wawili hao kuzuiliwa na polisi ambapo pia wamefikishwa mahakamani,bado hawajafunguliwa mashtaka wala kuombwa kujibu tuhuma wanazokabiliwa nazo.

Mabaki ya Rita Wdaeni wanafunzi mwenye umri wa miaka 20, yaligunduliwa yakiwa yametupwa kwenye mifuko ya taka katika nyumba ya kukodisha ya muda mfupi, mita chache kutoka katika mji mkuu, Nairobi, Januari 14.

Licha ya mabaki yake kupatikana, kichwa chake pamoja na simu yake ya mkononi hazikupatikana.

Mauaji hayo yamekuwa ya hivi punde kukashifiwa, wito ukitolewa kwa maofisa wa polisi kuanzisha uchunguzi zaidi kuwakamata wahusika na mauaji hayo ya kinyama.

Kando na raia hao wa Nigeria, Wakenya wanne pia wanashikiliwa na vyombo vya usalama kuhusiana na mauaji hayo, pamoja na mtu mmoja ambaye alikuwa akisafiri kwa pasipoti ya Msumbiji ambaye alikamatwa wakati akijaribu kuondoka nchini humo.

Kwa mujibu wa polisi, raia hao wa Nigeria ni William Ovie Opia na Johnbull Asbor.

Opia alikuwa na pasipoti ya Nigeria ambayo muda wake ulikuwa umekamilika wakati Asbor naye alikuwa amepoteza paspoti yake miaka miwili iliyopita.

Katika oparesheni ya kuwakamata washukiwa hao Polisi walinasa vitu kadhaa kutoka kwa nyumba yao ikiwa ni pamoja na kisu cha kukata nyama na shoka dogo linaloshukiwa kutumika katika mauaji ya mwanafunzi huyo wa chuo kikuu, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kenya vikiwanukuu polisi.

Opia aliwaeleza wachunguzi kwamba alinunua shoka hilo mtandaoni kwa ajili ya kujilinda, gazeti la kibinafsi la Nation liliripoti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.