Pata taarifa kuu

Kenya haipo vitani na jirani zake: Musalia Mudavadi

Nairobi – Mkuu wa mawaziri nchini Kenya, ambaye pia ni waziri wa mambo ya kigeni Musalia Mudavadi, amekanusha madai ya kushuka kwa ushusiano kati ya nchi yake na majirani zake.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Musalia Mudavadi.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Musalia Mudavadi. © Musalia Mudavadi
Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya waziri huyo yamekuja wakati huu kukiripotiwa kuwepo kwa mivutano kadhaa ambayo kwa mujibu wake inatatuliwa kwa njia za kidiplomasia.

Taifa hilo la Afrika Mashariki kwa sasa linakabiliwa na kesi kuhusu usafirishaji wa mafuta na jirani yake nchi ya Uganda licha ya wiki iliyopita kutatua mvutano kuhusu usafiri wa anga na Tanzania.

Mapema mwezi huu, nchi ya Sudan ilimuagiza balozi wake jijini Nairobi kurejea nyumbani baada ya Kenya kumpokea kiongozi wa wapiganaji wa RSF Mohamed Dagalo, ambaye kundi lake linapigana na uongozi wa kijeshi nchini Sudan.

Mwezi Desemba, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pia ilimwagiza balozi wake kurejea Kinshasa baada ya Nairobi baada ya kundi jipya la waasi kuzinduliwa katika ardhi ya Kenya.

Katika taarifa yake ya siku ya Jumapili, Mkuu huyo wa mawaziri alieleza kuwa nchi yake iko katika mstari wa mbele kuhakikisha usalama unapatikana kwenye nchi za ukanda na kusisitiza kuwa Nairobi haiko vitani na jirani zake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.