Pata taarifa kuu

Kenya: Serikali imetakiwa kukomesha visa vya mauaji ya wanawake

Nairobi – Mashirika ya kutetea haki za binadamu sasa yanaitaka Serikali ya Kenya, kuchukua hatua za makusudi kuanzisha uchunguzi na kuwashtaki watu wanaotuhumiwa kwa makosa ya mauaji na udhalilishaji dhidi ya wanawake, baada matukio ya hivi karibuni ambapo baadhi ya wanawake wameuawa kikatili.

Visa vya mauaji ya wanawake vimekuwa vikiripotiwa katika baadhi ya sehemu nchini Kenya
Visa vya mauaji ya wanawake vimekuwa vikiripotiwa katika baadhi ya sehemu nchini Kenya Getty Images/Tetra images RF - ac productions
Matangazo ya kibiashara

Mauaji ya hivi punde ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20, mwanafunzi wa chuo kikuu aliyeuawa kwa kukatakatwa vipande na wanaume wanaodaiwa kuwa walipanga kukutana kwenye nyumba moja ya wageni jijini Nairobi.

Kutokana na tukio, muasis wa shirika la kiraia linaloshugulikia masuala ya wanawake maarufu kama Femicide Count Kenya, Audrey Mugeni, ameitaka serikali kufanya zaidi kukomesha matukio haya.

Kwa mujibu wa shirika hilo, wanawake 152 wameuawa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, idadi inayotajwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa, Shirika hilo likionya kuwa huenda idadi ikawa ni kubwa zaidi hasa kutokana na baadhi ya matukio kutoropotiwa kwa idara za usalama.

Inadaiwa kuwa mwanamke mmoja kati ya watatu nchini Kenya, amethibitisha kudhulumiwa katika maisha yake kwa mujibu wa takwimu za kitaifa za mwaka wa 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.