Pata taarifa kuu

Kenya: Kiongozi wa dini anakabiliwa na mashtaka 10 ikiwemo mauaji

Nairobi – Mkurugenzi wa mashtaka nchini Kenya ,Renson Ingonga ameidhinisha mashtaka 10 dhidi ya mchungaji mwenye utata Paul Mackenzie , wa kanisa la Good news Internatioanal,anayetuhumiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 430 eneo la Shakahola ,pwani ya  nchi hiyo.

Baadhi ya mashtaka dhidi ya Mackenzie ni mauaji  na ugaidi mashtaka mengine yakiwa ni kuua bila kusudia na kusababisha majeraha ya mwili
Baadhi ya mashtaka dhidi ya Mackenzie ni mauaji  na ugaidi mashtaka mengine yakiwa ni kuua bila kusudia na kusababisha majeraha ya mwili REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

 

Kiongozi wa mashtaka amesema baada ya kutathmini faili ya uchunguzi kutoka idara ya upelelezi ,kuna ushahidi wa kutosha kumshtaki mchungaji Mackenzie na washirika wake 95 wanaohusishwa na vifo vya washirika wa kanisa hilo la kufunga hadi kufa.

Baadhi ya mashtaka dhidi ya Mackenzie ni mauaji  na ugaidi mashtaka mengine yakiwa ni kuua bila kusudia na kusababisha majeraha ya mwili.

Kwa mujibu wa sheria ya Kenya ya kuzuia ugaidi na uhalifu wa kupangwa,watuhumiwa hao watashtakiwa kwa kuhusika kwenye uhalifu wa kupangwa na mafunzo yenye itikadi kali.

Polisi walifukua miili zaidi ya 200 katika msitu wa Shakahola pwani ya Kenya
Polisi walifukua miili zaidi ya 200 katika msitu wa Shakahola pwani ya Kenya AP

Aidha chini ya sheria ya kuwalinda watoto ,Mackenzie na washirika wake watakabiliwa na kosa la ukatili dhidi ya watoto na ukiukaji wa haki ya kupata elimu.

Mackenzie na watuhumiwa wenzake wamekuwa korokoroni tangu mwezi mei mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.