Pata taarifa kuu

Mfalme Charles wa tatu wa Uingereza amekutana na rais Ruto jijini Nairobi

Nairobi – Mfalme wa Uingereza Charles wa tatu ameanza ziara ya siku nne nchini Kenya, ziara yake ya kwanza katika koloni ya zamani ya Uingereza.

Kiongozi huyo anafanya ziara ya siku nne nchini Kenya
Kiongozi huyo anafanya ziara ya siku nne nchini Kenya REUTERS - PHIL NOBLE
Matangazo ya kibiashara

Akiwa ameandamana na Malkia Camilla, Charles aliwasili katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki usiku  wa kuamkia leo ambapo amepokelewa na rais wa Kenya William Ruto katika Ikulu ya Nairobi.

Kasri la Buckingham imesema ziara hiyo ni ishara ya ushirikiano wa karibu kati ya nchi hizo mbili katika maendeleo ya kiuchumi, mabadiliko ya hali ya hewa na masuala ya usalama.

Baadhi ya mashirika ya kiraia yametoa kwa kiongozi huyo kuomba msamaha kutokana na yaliofanyika wakati wa ukoloni
Baadhi ya mashirika ya kiraia yametoa kwa kiongozi huyo kuomba msamaha kutokana na yaliofanyika wakati wa ukoloni REUTERS - PHIL NOBLE

Charles anatarajiwa pia kukutana na wajasiriamali kutoka eneo lenye shughuli nyingi za kiteknolojia nchini Kenya na kutembelea vituo vya wanyamapori.

Yeye na Camilla pia  watasafiri hadi kusini mashariki mwa mji wa bandari wa Mombasa.

Kiongozi huyo anafanya ziara ya siku nne nchini Kenya
Kiongozi huyo anafanya ziara ya siku nne nchini Kenya REUTERS - THOMAS MUKOYA

Wakenya wengi, hata hivyo, wanaangazia zaidi kile Charles atakachosema kuhusu dhuluma za wakati wa ukoloni, ikiwa ni pamoja na mateso, mauaji na kuenea kwa unyakuzi wa ardhi, ambayo sehemu kubwa bado inamilikiwa na  raia na makampuni ya Uingereza.

Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili
Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili REUTERS - THOMAS MUKOYA

Tume ya haki za kibinadamu nchini  Kenya (KHRC) imekadiria kuwa raia 90,000 wa Kenya waliuawa au kujeruhiwa vibaya na 160,000 kuzuiliwa wakati wa mapambano ya uhuru kati ya wapiganaji wa Mau Mau na serikali ya Uingereza wakati huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.