Pata taarifa kuu

Kenya: Rais Ruto amesaini kuwa sheria misawada ya kufanikisha afya kwa wote

Nairobi – Nchini Kenya, rais wa Kenya William Ruto Alhamis ya wiki hii, amesaini kuwa sheria miswada minne itakayofanikisha mpango wa afya kwa wote ambapo wafanyakazi wote watachangia asilimia 2.75 ya mishahara yao kufadhili mpango huo.

Wakenya wengi wameupinga baadhi wakiutazama kama ushuru mpya ambao ni wa juu, ukilinganisha na hali ngumu ya maisha kwa sasa
Wakenya wengi wameupinga baadhi wakiutazama kama ushuru mpya ambao ni wa juu, ukilinganisha na hali ngumu ya maisha kwa sasa © Wiliam Ruto
Matangazo ya kibiashara

Rais Ruto, amesema mfuko huo utahakikisha wakenya wote wanapata huduma za afya, ambapo wafanyikazi wote watachangia mfuko huo utakaochukua nafasi ya bima ya afya ya NHIF ambapo wakenya wamekuwa wakichangia kati ya shilingi 150 hadi 1700 kutibiwa katika hospitali za uma na binafsi.

Waziri wa afya Susan Nakhumicha, akipigia upatu mpango huo, amesema ni bora zaidi kwakuwa hautawabagua wakenya kwa msingi wa mapato yao.

Waziri wa afya nchini Kenya
Waziri wa afya nchini Kenya © Wiliam Ruto

Hata hivyo wakenya wengi wameupinga baadhi wakiutazama kama ushuru mpya ambao ni wa juu, ukilinganisha na hali ngumu ya maisha kwa sasa.

Rais Ruto, amesema mfuko huo utahakikisha wakenya wote wanapata huduma za afya
Rais Ruto, amesema mfuko huo utahakikisha wakenya wote wanapata huduma za afya © Wiliam Ruto

Mashirika ya kiraia pamoja wa wanaharakati wa huduma bora za afya pia wameukosoa mpango huo wanaosema hautaweza kukidhi mahitaji yote ya afya kutokana na mfumuko wa bei ambao umeathiri sekta zote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.