Pata taarifa kuu

Burundi : Mmoja wa viongozi wa upinzani anazuiliwa kwa kuhujumu usalama wa taifa

Nairobi – Mamlaka nchini Burundi zimemkamata mmoja wa viongozi wa upinzani Kefa Nibizi, wa chama cha (CODEBU), anayetuhumiwa kuhujumu usalama wa taifa.

Mji wa Bujumbura.
Mji wa Bujumbura. © Wikimedia
Matangazo ya kibiashara

Kwa mjibu wa vyanzo vya habari kutoka idara ya mahakama nchini Burundi, Nibizi alikamatwa baada ya chama chake kuonekana kuikosoa serikali, kupitia mtandao wa kijamii wa X, awali ukifahamika kama twitter.

Chama hicho juma lililopita kiliwataka raia wa Burundi kutovunjika moyo kutokana na kile kilitaja kuwa uongozi mbaya unaowasababishia raia mateso, na kuwataka kuiga mfano wa mwana Mfalme Luwii Rwaga-sore aliyekuwa kinara wa uhuru wa Burundi ambaye  aliyeuawa miaka 62 iliopita.

Chama cha CODEBU, kimetuhumu serikali kwa kumkamata kiongozi wake kikidai ujumbe wao ulieweka visivyo na kutaka Nibizi kuachialiwa mara moja.

Mashtaka ya Nibize yanawiana na yale ya alikuwa waziri mkuu wa zamani, Alain-Guillaume Bunyoni, ambaye pia anakabiliwa na mashtaka ya kuhujumu usalama wa taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.