Pata taarifa kuu

Uingereza: Serikali imesisitiza Rwanda ni eneo salama ya kuwapeleka wahamiaji

Nairobi – Serikali ya Uingereza, Jumatatu hii imesisitiza kuwa Rwanda ni sehemu salama ya kuwapeleka wahamiaji walionyimwa hifadhi, wakati huu London ikijaribu kubatilisha uamuzi wa awali wa mahakama ya rufaa ambayo ilisema mpango huo ni kinyume cha sheria.

Suala la wahamiaji huenda likawa ni suala mtambuka wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi wa mwakani
Suala la wahamiaji huenda likawa ni suala mtambuka wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi wa mwakani AFP - GLYN KIRK
Matangazo ya kibiashara

Kesi hii inasikilizwa baada ya mwezi Juni, majaji watatu wa mahakama ya rufaa kuzuia mpango wa Serikali wakisema Rwanda haiwezi kuhesabika kama nchi salama.

Kesi hii ambayo itadumu kwa Siku tatu, imeshuhudia mawakili wa serikali wakitetea mpango wa serikali ya waziri mkuu Rish Sunak, wakisema pamoja na kwamba Rwanda haivutii kama Uingereza, lakini bado nchi hiyo ni salama.

Utawala wa Kigali umeendelea kusisitiza nchi hiyo kuwa salama kwa wageni
Utawala wa Kigali umeendelea kusisitiza nchi hiyo kuwa salama kwa wageni AFP - SIMON WOHLFAHRT

Suala la wahamiaji huenda likawa ni suala mtambuka wakati huu nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi wa mwakani, ambapo Serikali inajaribu kuweka mikakati ya kudhibiti wimbi la wahamiaji.

Licha ya ukosolewaji wa mashirika ya kutetea haki za binadamu na yale ya umoja wa Mataifa, utawala wa Kigali umeendelea kusisitiza nchi hiyo kuwa salama kwa wageni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.