Pata taarifa kuu

Kenya: Deni kumpeleka rais Ruto China

Nairobi – Rais wa Kenya, William Ruto anatarajiwa kufanya ziara nchini China baadae mwezi huu akiwa na lengo kutafuta mkopo wa Dola bilioni moja kufadhili miradi iliyokwama, naibu wa rais Rigathi Gachagua amethibitisha.

Rais Ruto anatarajiwa kuzuru China baadae mwezi huu, Beijing ikiwa mkopoeshaji mkubwa wa Kenya
Rais Ruto anatarajiwa kuzuru China baadae mwezi huu, Beijing ikiwa mkopoeshaji mkubwa wa Kenya AP - Jeff Chiu
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na kituo cha redio cha Inooro kinachotagaza kwa lugha ya mama, naibu rais amesema wanakandarasi katika baadhi ya maeneo kwenye taifa hilo wamesusia kazi kwa kukosa kulipwa kutokana na kazi wanayofanya.

Naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua amesema serikali imepiga marafuku ziara za nje za maofisa wake ilikupunguza matumizi ya serikali
Naibu rais wa Kenya Rigathi Gachagua amesema serikali imepiga marafuku ziara za nje za maofisa wake ilikupunguza matumizi ya serikali AFP - YASUYOSHI CHIBA

Gachagua amesema kuwa licha ya kwamba Kenya inadaiwa na China, rais Ruto anatafuta mkopo zaidi wa Dola bilioni moja pamoja na kutafuta namna ya kulipia deni ambalo China inadai nchi yake.

Kenya inadaiwa na  China zaidi ya Dola bilioni 8 kutokana na mikopo inayodaiwa kutolewa wakati wa serikali ya zamani chini ya rais Uhuru Kenyatta kwa ajili ya miradi ya miundombinu.

Miundombinu mikubwa kama vile barabara ya juu jijini Nairobi imefadhiliwa na mkopo kutoka kwa serikali ya China
Miundombinu mikubwa kama vile barabara ya juu jijini Nairobi imefadhiliwa na mkopo kutoka kwa serikali ya China REUTERS - THOMAS MUKOYA

Naibu rais alizungumzia swala la ubadhirifu unaofanywa na maafisa wa serikali akisema hilo ndilo limesababisha rais kuagiza kuzuiliwa kwa safari za nje za maofisa wa serikali.

Mapema wiki hii, ofisi ya rais ilipiga marufuku maafisa wa umma kufanya safari zisizo za lazima nje ya nchi ili kubana matumizi na imeziagiza wizara zote kupunguza bajeti ya mwaka ujao wa fedha kwa asilimia 10.

Raia wa Kenya wamekuwa wakitoa kwa serikali ya rais William Ruto kutatua suala la kupanda kwa gharama ya maisha
Raia wa Kenya wamekuwa wakitoa kwa serikali ya rais William Ruto kutatua suala la kupanda kwa gharama ya maisha AP - Ludovic Marin

Serikali imeshutumiwa kwa matumizi yasiyo ya lazima wakati huu raia wa taifa hilo wakikerwa kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha na nyongeza ya ushuru iliyotangazwa na serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.