Pata taarifa kuu

Kenya: Rais Ruto atekeleza mageuzi katika baraza la mawaziri

Nairobi – Rais wa Kenya William Ruto ametekeleza mabadiliko kwenye baraza la mawaziri na kuiweka wizara ya mashauri ya nchi za kigeni chini ya ofisi ya mkuu wa mawaziri.

Haya yanajiri baada ya rais kuwakosoa mawaziri wake hadharani hivi majuzi, akiwashutumu baadhi yao kwa kutokuwa na ufahamu kuhusu nyadhifa zao
Haya yanajiri baada ya rais kuwakosoa mawaziri wake hadharani hivi majuzi, akiwashutumu baadhi yao kwa kutokuwa na ufahamu kuhusu nyadhifa zao AP - Jeff Chiu
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri baada ya rais kuwakosoa mawaziri wake hadharani hivi majuzi, akiwashutumu baadhi yao kwa kutokuwa na ufahamu kuhusu nyadhifa zao.

Rais Ruto anasema mabadiliko hayo yanalenga kuboresha utendakazi na kuimarisha utoaji wa huduma kama ilivyoainishwa katika manifesto yake.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni sasa itaongozwa na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, huku waziri wa awali Alfred Mutua akiongoza wizara ya utalii.

Pia walioathirika ni aliyekuwa waziri wa biashara Moses Kuria, ambaye sasa ataongoza wizara ya utumishi wa umma.

Kuria siku za hivi majuzi amekuwa akikosolewa kwa kile ambacho kimeonekana kuwa mbinu yake inayodaiwa kuwa ya kiburi wakati wa kushughulikia gharama ya juu ya maisha nchini Kenya.

Awali alizua utata kuhusu matamshi yake dhidi ya duka linalomilikiwa na Wachina linalouza bidhaa za bei nafuu za nyumbani nchini Kenya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.