Pata taarifa kuu

Uganda: Wapenzi wa jinsia moja wanabaguliwa: Ripoti

Nairobi – Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda, yametoa ripoti kuonesha ongezeko la vitendo vya ukatili na ubaguzi dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja, tangu nchi hiyo ilipopitisha sheria tata kuhusu ushoga.

Matukio ya ubaguzi zaidi ya 300 yaliripotiwa kati ya Januari na Agosti mwaka huu
Matukio ya ubaguzi zaidi ya 300 yaliripotiwa kati ya Januari na Agosti mwaka huu AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashirika hayo, tangu sheria hiyo ilipotiwa saini na rais Yower Museveni mwezi Mei mwaka huu, watu 6 wameripotiwa kushtakiwa chini ya sheria hii mpya, ambayo adhabu ya juu ni kifo.

Aidha ripoti hii ambayo imeandaliwa na shirika la Convening for Equality, imesema watekelezaji wakubwa wa vitendo hivi dhidi ya mashiga ikiwemo ubakaji, mateso na ukatili mwingine, ni watu binafsi.

Waandishi wa ripoti hiyo wamesema kuongezeka kwa vitendo hivi kumechangiwa na namna sheria ilivyotengenezwa, ambapo inahamasisha ubaguzi dhidi ya kundi hilo.

Matukio zaidi ya 300 yaliripotiwa kati ya Januari na Agosti mwaka huu, huku mwaka 2020 na 2021 asilimia 70 ya vitendo vya ukiukaji haki za binadamu vilitekelezwa na idara za usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.