Pata taarifa kuu

Uganda: Maandalizi ya tamasha la Nyege Nyege yapingwa mjini Jinja

Viongozi nchini Uganda, wamekosa kukubaliana kuhusu maandalizi ya tamasha maarufu la Nyege Nyege katika mji wa Jinja Mashariki mwa taifa hilo, tamasha ambalo wanalolipinga wanadai linakwenda kinuyme na maadili.

Viongozi hao wanasema tamasha hilo linakwenda kinuyme na maadili ya jamii
Viongozi hao wanasema tamasha hilo linakwenda kinuyme na maadili ya jamii © RFI/Lucie Mouillaud
Matangazo ya kibiashara

Nyege Nyege, ni tamsha la muziki la kila mwaka ambalo limekuwa likiandaliwa nchini Uganda tangu mwaka wa 2015 na ni mojawapo ya tamasha maarufu kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki na ambalo limezua hisia tofauti kutoka wa raia wa Afrika Mashariki.

Baadhi ya viongozi wa kiisilamu katika mji wa Jinja wakiongozwa na Kadhi wa wilaya ya Jinja Sheikh Ismail Basoga Adi, wamepinga kufanyika kwa tamasha hilo kwenye mji huo.

Viongozi wa kiisilamu wanapinga maandalizi ya tamasha hilo mjini Jinja
Viongozi wa kiisilamu wanapinga maandalizi ya tamasha hilo mjini Jinja AFP - BADRU KATUMBA

Kwa upande wake waziri wa masuala ya Afrika Mashariki nchini Uganda, Alitwala Kadaga, amekashifu hatua hiyo ya viongozi waisilamu kupinga tamasha hilo, akiawataja kama wabinafasi wanaojificha nyuma ya dini.

Waziri huyo amesema tamasha hilo halifai kusitishwa kwa sababu watoto hawaruhusiwi kuhudhuria na kwamba viongozi hao wa kiisilamu hawajawahi pinga maandalizi ya tamsha kama hilo kwenye mji huo awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.