Pata taarifa kuu

Kenya: Pendekezo la kuongeza muhula wa rais lazua mjadala

Nchini Kenya hatua ya seneta aliyetuliwa kwa tiketi ya chama tawala, kupendekeza kuongezwa kwa muda wa rais kuhudumu kutoka miaka mitano hadi saba imezua hisia mseto kutoka wa raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Katiba ya Kenya imeweka kikomo cha urais wa mihula miwili na mabadiliko yoyote yatahitaji kufanyika kwa  kura ya maoni
Katiba ya Kenya imeweka kikomo cha urais wa mihula miwili na mabadiliko yoyote yatahitaji kufanyika kwa  kura ya maoni AP - Ludovic Marin
Matangazo ya kibiashara

Seneta wa Nandi, katika mkoa wa bonde la ufa Samson Cherargei, anasema rais  William Ruto, ambaye amekuwa afisini kwa kipindi cha mwaka moja peke, huenda akakosa muda wa kutosha kuwahudumia Wakenya kwa mujibu wa yale aliyowahidi wakati wa kampeni za mwaka wa 2022.

Pendekezo hilo hata hivyo limekashifiwa kutoka wa upinzani na baadhi ya wakenya wanaoituhumu serikali kwa kupanga njama ya kutupilia mbali hitaji la kuwataka marais kuongoza kwa mihula.

Mwezi Novemba mwaka uliopita, rais Ruto alitupilia mbali mapendekezo ya mbunge mwengine wa chama chake aliyekuwa anataka kuondolewa kwa hitaji la mihula.

Katiba ya Kenya imeweka kikomo cha urais wa mihula miwili na mabadiliko yoyote yatahitaji kufanyika kwa  kura ya maoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.