Pata taarifa kuu

Burundi: Rais Ndayishimiye akashifu taarifa za uongo kuhusu mapinduzi dhidi yake

Nairobi – Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye, amekashifu kile ambacho amesema ni habari za kupotosha kuhusu kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi kwenye taifa lake wakati akiwa nje ya nchi kwa kipindi cha wiki mbili.

Hadi sasa chanzo cha taarifa hizo za kupotosha bado hakijatambuliwa
Hadi sasa chanzo cha taarifa hizo za kupotosha bado hakijatambuliwa AFP - TCHANDROU NITANGA
Matangazo ya kibiashara

Rais Ndayishimiye amekuwa nchini Cuba kwa ziara na kuzuru pia kule nchini Marekani ambako alihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New York.

Siku moja baada ya kiongozi huyo wa nchi kuondoka nchini mwake tarehe 10 ya mwezi Septemba, taarifa ziliaanza kusambaa katika mitandao ya kijamii zikidai kuwepo kwa njama ya kutekelezwa kwa mapinduzi dhidi yake.

Hadi sasa chanzo cha taarifa hizo za kupotosha bado hakijatambuliwa.

Katika hotuba yake baada ya kurejea jijini Bujumbura usiku wa Jumapili ya wiki iliyopita, rais Ndayishimiye alihusisha taarifa hizo za kupinduliwa kwa serikali yake na watu ambao alisema walikuwa wanataka kuharibu sifa ya taifa la Burundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.