Pata taarifa kuu

Burundi na harakati za kuwakabili waasi nchini DRC

Nairobi – Burundi imeendelea kuwa na mikataba ya siri ya ushirikiano wa kijeshi na nchi jirani ya DRC. Kikosi cha Burundi kimeendeleza mapambano dhidi ya waasi wa RED Tabara na FNL katika mkoa wa Kivu Kusini.

Mwezi Agosti, rais Evariste Ndayishimiye aliziru Kinshasa na kusaini mkataba mpya wa ushirikiano wa kijeshi
Mwezi Agosti, rais Evariste Ndayishimiye aliziru Kinshasa na kusaini mkataba mpya wa ushirikiano wa kijeshi © Photo presidence de la République
Matangazo ya kibiashara

Imeripotiwa kuwa, Burundi chini ya kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki imetuma wanajeshi wake 3200 nchini DRC, lakini kikosi kingine huko Kivu Kaskazini kwa ombi la serikali ya  Kinshasa.

DRC inasema inawaamini zaidia wanajeshi wa Burundi kwenye mapambano dhidi ya waasi hasa wale wa M 23. Katika siku zilizopita, Kinshasa imeshtumu wanajeshi wengine kwenye kikosi cha Jumuiya kwa kushirikiana na waasi hao.

Mwezi Agosti, rais Evariste Ndayishimiye alizuru Kinshasa na kusaini mkataba mpya wa ushirikiano wa kijeshi, ambao umewezesha kutumwa kwa wanajeshi wengine 800 wa Burundi jimboni Kivu Kusini.

Ushirikiano wa kijeshi kati ya Burundi na DRC una historia ndefu, una ulianza wakati wa uongozi wa rais wa zamani Joseph Kabila, lakini pia waasi wa zamani wa Kihutu wa CNDD-FDD ambao kwa sasa wanaongoza Burundi, waliungana na DRC wakati wa vita vya kwanza na vya pili vya Congo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.