Pata taarifa kuu

Raia wa Kenya wakerwa na hatua ya serikali kuongeza bei ya mafuta

Nairobi – Wakenya wamegadhabishwa na hatua ya serikali kuongeza bei ya mafuta, wakati huu raia wengi wanapoendelea kupitia kipindi kigumu cha kiuchumi.

Nchini Kenya kama ilivyo katika mataifa mengine duniani, bei ya mafuta inapopanda, husababisha pia kupanda kwa bei ya bidhaa hasa chakula na usafiri
Nchini Kenya kama ilivyo katika mataifa mengine duniani, bei ya mafuta inapopanda, husababisha pia kupanda kwa bei ya bidhaa hasa chakula na usafiri REUTERS - Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka inayodhibit bei ya nishati nchini humo EPRA, usiku wa kuamkia Ijumaa ilitangaza bei hiyo mpya, na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo, Lita Moja wa mafuta inauzwa Shilingi za Kenya 211 sawa na Dola Moja na Senti 40.

Hatua hii imekuja licha ya maandamano ya miezi kadhaa, ilitokea huko nyuma, kupinga será za kiuchumi za serikali ya rais William Ruto, ambazo wananchi wengi wanalalamikia, kuwa zimesababisha maisha kuwa magumu.

Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani wakati wa maandamano yaliofanyika jijini Nairobi kupinga kupanda kwa gharama ya maisha awali
Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani wakati wa maandamano yaliofanyika jijini Nairobi kupinga kupanda kwa gharama ya maisha awali REUTERS - JOHN MUCHUCHA

Serikali ya Ruto ambayo ilitoa ruzuku ya mafuta baada ya kuingia madarakani mwezi Septemba mwaka uliopita, inasema ongezeko hili ni kutokana na mwenendo wa bei ya mafuta kwenye soko la Kimataifa.

Mshauri wa masuala ya kiuchumi wa rais Ruto, David Ndii kwenye ukurasa wake wa X, amewambia Wakenya wajiandae kwa kujiandaa kwa nyakati ngumu.

Nchini Kenya kama ilivyo katika mataifa mengine duniani, bei ya mafuta inapopanda, husababisha pia kupanda kwa bei ya bidhaa hasa chakula na usafiri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.