Pata taarifa kuu

Jeshi la Uganda na DRC kuendelea na oparesheni dhidi ya ADF

Nairobi – Jeshi la Uganda na lile la DRC wamekubaliana kuendelea na oparesheni dhidi ya Allied Democratic Forces (ADF) kwa miezi mingine minne.

Jeshi la  FARDC limekuwa likipambana na makundi ya waasi mashariki ya taifa hilo ikiwemo ADF
Jeshi la FARDC limekuwa likipambana na makundi ya waasi mashariki ya taifa hilo ikiwemo ADF © Sebastien Kitsa Musay / AFP
Matangazo ya kibiashara

Oparesheni hiyo ilianza Desemba 2021 na ilitarajiwa kudumu kwa miezi 6 pekee.

Uamuzi wa kuongeza muda wa operesheni hiyo ulitangazwa baada ya ujumbe wa wanajeshi wa DRC ukiongozwa na Luteni Jenerali Christian Tshiwewe Songesa kukutana na kamanda wa jeshi la Uganda Jenerali Wilson Mbasu Mbadi ili kupitia kile kilichotokea hadi sasa.

Kulingana na taarifa kutoka UPDF, miezi minne ijayo italenga kuunganisha mafanikio yaliyopatikana na kuondoa makundi yote yaliyojitenga ya ADF.

Mwezi Julai , mazishi za baadhi ya watu 42 wengi wao wanafunzi wa shule ya sekondari waliouawa baada ya kushambuliwa na waasi wa ADF mwishoni mwa wiki iliyopita katika mji wa Mpondwe, nchini Uganda karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yalifanyika, huku wakaazi wa eneo hilo, wakihofia usalama wao.

ADF linaonekana kuwa tishio baada ya ripoti ya umoja wa mataifa kuonesha ADF imekuwa ikifadhiliwa na kundi la Kijihadi la Islamic State tangu mwaka 2019.

Kuna hofu kuwa mtandao ADF unaweza kusambaaa zaidi baada ya ripoti hiyo kusema Islamic State imekuwa ikiwatumia watu kutoka mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.