Pata taarifa kuu

Magaidi wa Al Shabab wametekeleza shambulio Lamu, pwani ya Kenya

Nairobi – Nchini Kenya, watu wawili wameuawa na nyumba nane kuteketezwa moto, likiwemo Kanisa moja, baada ya magaidi wa Al Shabab katika Kaunti ya Lamu, Pwani ya nchi hiyo. hapo jana Jumanne.

Wapiganaji wa Al Shabab wamekuwa wakituhumiwa kwa kutekeleza mashambulio katika kaunti jirani na Somalia
Wapiganaji wa Al Shabab wamekuwa wakituhumiwa kwa kutekeleza mashambulio katika kaunti jirani na Somalia Feisal Omar/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Akithibitisha tukio hilo, naibu wa Kamishna kaunti ya Lamu Gabriel Kioni, amesema wanamgambo hao waliwavamia wakaazi eneo la Salama na kuteketeza nyumba nane, pamoja na kutekeleza uharibifu.

‘‘Waliweza kuharibu chakula ambacho kwa sasa hatujui ni kiasi gani lakini pia waliweza kubeba chakula kingine, na vilevile mifugo mbuzi kama saba pamoja na kuuwa mbuzi wengine.’’alisemanaibu wa Kamishna kaunti ya Lamu Gabriel Kioni.

00:11

Naibu wa Kamishna kaunti ya Lamu Gabriel Kioni

Wakaazi wa eneo hilo na walikuwa na haya ya kusema.

‘‘Magaidi wakaja wakatuvamia kuchoma manyumba kama kwangu wamevuna mahindi na wakachoma kila kitu.’’Alisema mmoja wa wakaazi wa eneo husika.

 

00:14

Wakaazi wa kaunti ya Lamu pwani ya Kenya

 

Kasisi Muthegi ni kiongozi wa kanisa ambalo liliteketezwa na magaidi hao.

‘‘Wamechoma Bibilia nyingi na vitabu vya kuweka rekodi za kanisa, wamechoma mpaka hata mafungo ambayo huwa tunaweka hapa.’’alieleza Kasisi Muthegi.

00:06

Kasisi Muthegi ni kiongozi wa kanisa ambalo liliteketezwa na magaidi hao

Naibu wa Kamishna Gabriel Kioni aliongezea kusema kuwa wanamgambo hao pia walijaribu kuvamia kambi ya jeshi eneo la Pandanguo bila mafanikio, na kisha wakaenda kutekeleza mauaji ya watu wawili barabarani.

‘‘Walienda pia wakavamia kituo cha jeshi lakini hawakufaulu kupenya wakazidiwa nguvu, baada ya hapo pale sehemu ya Nyongoro, waliweza kusimamisha lori na wakauwa watu wawili dereva na kondakta wake.’’ aliongeza naibu wa Kamishna Gabriel Kioni.

Watu wanaodhaniwa kuwa ni magadi kutoka nchi jirani ya Somalia, wamekuwa wakitekeleza mashambulio katika kaunti jirani na Kenya kwa muda sasa.

Kwa sasa idara ya usalama katika kaunti hiyo ya Lamu imewataka raia kuwa waangalifu pamoja na kutoa ushirikiano kwa walinda usalama kwa kutoa habari zitakazowasaidia.

Diana Wanyonyi- Mombasa RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.