Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa Uganda na DR Congo wamewaokoa abiria waliokuwa wametekwa

Nairobi – Muungano wa majeshi ya Uganda na yale ya Serikali ya DRC, juma hili umefanikiwa kuwaokoa abiria 17 waliokuwa wametekwa nyara na waasi wa ADF Jumatano ya wiki hii katika milima ya Kamungu, barabara ya Eringeti na Kianama, jimboni Kivu kaskasini.

Wanajeshi wa Uganda, wamekuwa wakisaidiana na jeshi la Congo tangu Novemba mwaka 2021.
Wanajeshi wa Uganda, wamekuwa wakisaidiana na jeshi la Congo tangu Novemba mwaka 2021. AFP - SEBASTIEN KITSA MUSAYI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashirika ya kiraia wilayani Beni, abiria hao walitekwa nyara wakati wakirejea kutoka soko la Kainama kuelekea Eringeti ambapo walikuwa wakitumia magari na pikipiki walipovamiwa na waasi hao.

Msemaji wa kikosi hicho Mak Hazukay, amesema 17 hao wengi wakiwa wafanyabiashara, kwa sasa wako kwenye mikono salama ya idara ya usalama huko Kainama, wakisubiri kuunganishwa na família zao.

Waasi hao walichoma moto magari na pikipiki tatu zilizokuwa zinatumika na wafanyibiashara hao ,na kuwateka abiria huku wakiwaacha madereva  .

Hazukay, amewataka, wote wanaotaka kutumia barabara hiypo ambayo hadi sasa bado kurejea katika hali ya kawaida, kupata maelekezo kutoka wanajeshi wanaoshika doroa kabla kuanza safari.

Wanajeshi wa Uganda, wamekuwa wakisaidiana na jeshi la Congo tangu Novemba mwaka 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.