Pata taarifa kuu

Kenya: Ruto aonya mawaziri wanaochelewa kwenye vikao

Nairobi – Nchini Kenya, Rais William Ruto ameelezea kuchukizwa na hatua ya kuchelewa kwa baadhi ya mawaziri wake wakati wa kikao cha baraza la mawaziri mapema leo Jumanne katika Ikulu ya Nairobi na kuwataka waliochelewa kuwasilisha maelezo kwa maandishi.

Rais Ruto amewataka mawaziri wake kufanya kazi kwa uadilifu na uwazi
Rais Ruto amewataka mawaziri wake kufanya kazi kwa uadilifu na uwazi © Statehouse Kenya
Matangazo ya kibiashara

Rais Ruto amekuwa akiongoza hafla ya kutia saini kandarasi za utendakazi kwa maofisa wake ambapo baadhi walichelewa kuwasili kama ilivyokuwa imeratibiwa.

Miongoni mwa wale walioripotiwa kuchelewa kufika kwenye kikao ni pamoja na waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki na waziri wa biashara Moses Kuria ambao hawakushiriki kwenye hafla hiyo  kutia saini kandarasi za utendakazi.

Mkuu wa nchi ameeleza kuwa viongozi waliopewa jukumu la kuwatumikia raia wa Kenya wanapaswha kufanya kazi kwa uadilifu.

Ruto ambaye alionekana na kukerwa alisisitiza kuwa anashikilia kwa dhati masuala yanayohusiana na utoaji huduma na yeyote anayeshughulikia masuala ya kitaifa bila kujali atawajibishwa.

Kandarasi wa utendakazi serikalini zinatumika kama kigezo cha kupima utendakazi wa wizara na mashirika katika kuwahudumia Wakenya.

Rais Ruto ameongoza zoezi hilo katika Ikulu ya Nairobi
Rais Ruto ameongoza zoezi hilo katika Ikulu ya Nairobi © Statehouse Kenya

Aidha mkuu wa nchi amewaonya maofisa wa umma dhidi ya kujihusisha na vitendo vya ufisadi na kuwataka kuwajibikia majukumu yao.

Aliwakosoa  mawaziri ambao mara kwa mara walisafiri nje ya nchi, na kuzuia utendakazi wa kamati za baraza la mawaziri. 

Naibu rais Rigathi Gachagua naye pia amewataka mawaziri kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia muda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.