Pata taarifa kuu

Haiti yakaribisha pendekezo la Kenya kujitolea kuongoza kikosi kimataifa

Nairobi – Haiti imekaribisha kwa shauku kubwa pendekezo la Kenya kujitolea kuongoza kikosi cha wanajeshi 1,000 wa kimataifa ili kuimarisha usalama katika nchi hiyo iliyokumbwa na ghasia.

Maofisa wa usalama nchini Haiti wamekuwa wakipambana na magenge ya watu wenye silaha kwa muda sasa hali inayotishia usalama wa kitaifa
Maofisa wa usalama nchini Haiti wamekuwa wakipambana na magenge ya watu wenye silaha kwa muda sasa hali inayotishia usalama wa kitaifa AP - Odelyn Joseph
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya nje wa Haiti, Jean Victor Geneus kwenye taarifa amesema kwamba nchi yake inathmini kitendo hiki cha mshikamano wa Afrika huku pia akisema anatazamia kukaribisha ujumbe wa Kenya wa tathmini hali ilivyo.

Siku ya Jumamosi, Kenya ilitangaza kuwa tayari kuwatuma polisi 1000 ili kutoa mafunzo na kusiadia wenzao wa Haiti katikakukabiliana na magengeya majambazi ambao wameendelea kuvurugha usalama wa mji mkuu wa Port-au-Prince.

Haiti imekaribisha kwa shauku kubwa pendekezo la Kenya kujitolea kuongoza kikosi cha wanajeshi 1,000 wa kimataifa ili kuimarisha usalama katika nchi hiyo iliyokumbwa na ghasia
Haiti imekaribisha kwa shauku kubwa pendekezo la Kenya kujitolea kuongoza kikosi cha wanajeshi 1,000 wa kimataifa ili kuimarisha usalama katika nchi hiyo iliyokumbwa na ghasia AP - Odelyn Joseph

Hata hivyo, Kenya kupeleka kikosi chake nchini Haiti, bado itahitaji idhini ya baraza la usalama la umoja wa mataifa, lakini pia makubaliano rasmi na mamlaka za Haiti.

Waziri wa mambo ya nje wa kenya, Dkt Alfred Mutua, amesema kuwa katika wiki zaijazo, Kenya itatuma ujumbe wa kutathmini hali ilivyo nchini Haiti.

Hatua ya Kenya inakuja wakati ambapo wanadiplomasia wa Marekani wamekuwa wakitafuta nchi itakayoongoza kikosi cha kimataifa nchini Haiti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.