Pata taarifa kuu

EU yatangaza vikwazo kwa raia tisa wa Rwanda na DRC

Nairobi – Umoja wa Ulaya, umewawekea vikwazo raia tisa wa DRC na Rwanda wanaotuhumiwa kuchangia utovu wa usalama na ukiukwaji wa haki za binadamu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waasi wa M23 na makundi mengine wamekuwa wakituhumiwa kwa utovu wa usalama mashariki mwa DRC
Waasi wa M23 na makundi mengine wamekuwa wakituhumiwa kwa utovu wa usalama mashariki mwa DRC AP - Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Waliowekewa vikwazo hivyo ni pamoja na viongozi wa makundi ya waasi ya M23, Twirwaneho, ADF na APCLS.

Wengine waliolengwa ni wale wanaoongoza makundi ya waasi ya CODECO/ALC, FDLR/FOCA pamoja na afisa mmoja wa jeshi la DRC na mwingine kutoka jeshi la Rwanda.

Aidha, Umoja wa Ulaya umesema, idadi ya watu waliowekewa vikwazo kwa kuendelea kusabisha utovu wa usalama na kujaribu kutatiza uchaguzi wa DRC uliopangwa kufanyika mwezi Desemba, imefikia 24.

Vikwazo walivyowekewa ni pamoja na kuzuiwa kusafiri barani Ulaya na mali zao kuzuiwa. Raia wa Umoja wa Ulaya na kampuni katika umoja huo, wamezuiwa kutoa fedha kwa watu hao.

Hatua hii inakuja wakati huu DRC ikiedelea kuishtumu Rwanda kwa kutumia waasi wa M 23 kudhoofisha hali ya usalama Mashariki mwa nchi yake, madai ambayo Kigali imeendelea kukanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.