Pata taarifa kuu

Kenya: Mahakama ya Rufaa yaidhinisha sheria ya fedha yenye utata ya mwaka wa 2023

Nairobi – Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imeruhusu kutekelezwa kwa Sheria ya Fedha ya mwaka wa 2023.

Rais wa Kenya William Ruto alitia saini muswada wa fedha 2023 kuwa sheria
Rais wa Kenya William Ruto alitia saini muswada wa fedha 2023 kuwa sheria © Statehouse Kenya
Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu ilikuwa imesitisha utekelezwaji wa sheria hiyo tarehe 30 ya mwezi Juni mwaka huu.

Hatua hii sasa inatoa nafasi kwa serikali kuaanza kuwatoza Wakenya ushuru tata uliokuwa umeidhinishwa na bunge katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa uamuzi wa majaji watatu wa mahakama hiyo ya Rufaa, serikali ya Kenya imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya kulipa mishahara wakati sheria hiyo ikiwa imesitishwa.

Rais wa Kenya William Ruto alitia saini kuwa sheria mswada wa kuongeza ushuru kwa bidhaa mbalimbali, na kukaidi ukosoaji kwamba hatua hiyo itawaongezea matatizo zaidi ya kiuchumi kwa wananchi wa taifa hilo.

Raia wa Kenya wamekuwa wakitoa kwa serikali ya Ruto kushugulikia suala la kupanda kwa gharama ya maisha
Raia wa Kenya wamekuwa wakitoa kwa serikali ya Ruto kushugulikia suala la kupanda kwa gharama ya maisha REUTERS - MONICAH MWANGI

Mpango huo mpya wa ushuru uliidhinishwa na bunge nchini humo unalenga kuongeza ushuru maradufu hadi asilimia 16 na kuanzisha kwa makato yanayolenga kuekelezwa kwa mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu, hatua inayotarajiwa kuwa na athari za kiuchumi kwa taifa hilo linalokabiliwa na mfumuko wa bei za bidhaa.

Ruto ambaye aliingia madarakani Septemba baada ya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali, analenga kujaza hazina ya serikali iliyopungua na kukarabati uchumi wenye madeni makubwa uliorithiwa kutoka kwa mtangulizi wake Uhuru Kenyatta, ambaye aliingia katika miradi mikubwa ya miundombinu.

Sheria hii mpya inatarajiwa kuongeza mapato ya nchi hadi kufikia dola bilioni 2.1 ambapo kodi ya bidhaa muhimu kama chakuma, miamala ya simu na huduma nyingine itaongezwa.

Upinzani nchini Kenya umekuwa ukisema sheria hiyo inalenga kuwaongezea mzigo raia ambao tayari wanakabiliwa na hali ngumu ya uchumi
Upinzani nchini Kenya umekuwa ukisema sheria hiyo inalenga kuwaongezea mzigo raia ambao tayari wanakabiliwa na hali ngumu ya uchumi © REUTERS/Thomas Mukoya

Hata hivyo moja ya kodi iliyoibua mjadala ni ile ya makazi nafuu, ambapo wafanyakazi nchini humo watakuwa wakikatwa asilimi 1.5 ya mshahara kila mwezi, ambapo pia muajiri atalipa kiasi sawa.

Kodi nyingine mpya ni ile ya asilimia tano ya maudhui ya watu wenye ushawishi mtandaoni.

Upinzani unaoongozwa na mpinzani wa Ruto, Raila Odinga umekuwa unapinga sheria hiyo mapya ukisema itaathiri mapato ya raia wa taifa hilo ambayo tayari yamebanwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.