Pata taarifa kuu

Kenya na China kushirikiana zaidi kimaendeleo

Nairobi – Kenya inalenga kuimarisha uhusiano wake na China ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini humo.

Rais wa Kenya William Ruto amekutana na mjumbe maalum wa China Wang Yi
Rais wa Kenya William Ruto amekutana na mjumbe maalum wa China Wang Yi © Statehouse Kenya
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Kenya, William Ruto, amesema Serikali yake itashirikiana kwa karibu na China katika maendeleo ya miundombinu, mabadiliko ya tabianchi, elimu na usalama.

Ruto amesema Kenya inalenga kuboresha barabara zake  chini ya jukwaa la ushirikiano wa China na Afrika.

Kiongozi huyo wa Kenya alikuwa  akizungumza Jumamosi katika Ikulu ya Nairobi, wakati wa mkutano wa ngazi ya juu na Wang Yi, mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkurugenzi wa ofisi ya kamati kuu ya kasuala ya kigeni.

Kenya na China zinalenga kufanya kazi kwa pamoja katika sekta za uchumi na ujenzi wa barabara
Kenya na China zinalenga kufanya kazi kwa pamoja katika sekta za uchumi na ujenzi wa barabara © Statehouse Kenya

Mkuu wa nchi ameeleza kuwa Serikali inapanga kuboresha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) na bandari za Mombasa na Lamu.

Aliwahakikishia wawekezaji wa China juu ya lengo la  Serikali yake kutoa usalama kwa kila mtu.

Kenya inalenga kunufaika na ujuzi wa China katika ujenzi wa barabara
Kenya inalenga kunufaika na ujuzi wa China katika ujenzi wa barabara © Statehouse Kenya

Kwa uapnde wake Yi amesema China itaendelea kufanya kazi na Kenya kwa ajili ya ustawi wa nchi hizo mbili.

Yi alieleza kuwa serikali ya China inaunga mkono kikamilifu utawala wa Rais Ruto na kumwalika kuzuru Beijing.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.