Kenya: Maandamano ya upinzani yaingia siku ya pili, watu sita wakiripotiwa kuuawa
Watu sita wameripotiwa kupoteza maisha katika maandamano ya siku tatu yaliyoanza Jumatano ya wiki hii nchini Kenya, kupinga kile upinzani unasema ni kupanda kwa gharama ya maisha, huku wizara ya mambo ya ndani ikithibitisha kukamatwa kwa waandamanaji zaidi ya 300.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Katika mitaa yenye wafuasi wengi wa upinzani kama Mathare na Kibera jijini Nairobi, polisi walitumia vitoza machozi kuwasambaratisha waandamanaji, huku kukiwa na ripoti ya baadhi watu waliojitkeza kuandamana wakijeruhiwa kwa kupigwa risasi.
Katika mwa jiji la Nairobi, athari za maandamano zimeshuhudiwa, maduaka yalifungwa na kinyume na siku nyingine hapakuwa na msongamano wa magari.
“Kwa kweli hakuna kitu tumeuza kwa sababu hakuna mtiririko wa watu.” Alisema Abadalla raia wa Kenya.
Abdalla, raia wa Kenya kuhusu maandamano
Baadhi ya raia wameonekan kuunga mkono maandamano haya huku wengine wakipinga.
“Hatuwezi zungumza maneno ya serikali wakati ambapo hata mwaka moja haujaisha, tusubiri mwaka ukamilike ndiyo tuone matokeo yake.” alisema mmoja wa wakaazi wa Nairobi.
Raia wa Kenya kuhusu maandamano
Maandamnao hayo yanaendelea tena hii leo Alhamis na kesho Ijumaa na muungano wa upinzani Azimio la Umoja, katika taarifa yake iliyotiwa saini na Martha Karua, naibu kiongozi wa muungano huo ameshtumu polisi kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji na kuwakamata baadhi ya viongozi wa upinzani, wakiwemo wabunge.
George Ajowi- RFI-Kiswahili Nairobi