Pata taarifa kuu

Kenya: Shule za kutwa zafungwa wakati huu maandano ya upinzani yakitarajiwa

Nairobi – Serikali ya Kenya Jumanne ya wiki hii, ilitangaza kufungwa kwa shule za kutwa katika mji mkuu na maeneo mengine mawili siku ya Jumatano wakati huu taifa hilo la Afrika Mashariki likijiandaa kwa siku tatu za maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha,maandamano ambayo rais amesema hataruhusu yafanyike.

Serikali ya Kenya inasema imechukua hatua ya kufunga shule kwa ajili ya usalama wa wanafunzi
Serikali ya Kenya inasema imechukua hatua ya kufunga shule kwa ajili ya usalama wa wanafunzi REUTERS - JOHN MUCHUCHA
Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya awali ya mwezi huu yalisababisha vurugu wakati polisi walipofyatua gesi ya kutoa machozi, watu 15 wakiripotiwa kuawaua kwa kupigwa risasi,mamia ya wengine wakithibitishwa kukamatwa.

Upinzani nchini Kenya uliitisha maandamano kutokana na nyongeza ya kodi iliyopitishwa mwezi uliopita na serikali ya Rais William Ruto, ambaye alichaguliwa Agosti mwaka jana akiahidi kusimamia maslahi ya maskini, lakini hilo limeonekana kuwa kinyume, bei za bidhaa za msingi zikipanda chini ya utawala wake.

Seŕikali inasema ushuru wa mafuta na nyumba, ambao unataŕajiwa kuongeza shilingi bilioni 200 (dola bilioni 1.4) kwa mwaka, zinahitajika kusaidia kukabiliana na kuongezeka kwa ulipaji wa madeni na kufadhili mipango ya kuunda nafasi za kazi.

Makanisa na mashirika ya kutetea haki za kiraia yamemtaka Ruto na kiongozi upinzani Raila Odinga kutatua tofauti zao kupitia mazungumzo na kusitisha maandamano hayo.

Siku ya Ijumaa Ruto alimshutumu Odinga kwa kujaribu kuibua hali ya kutoridhika na hali ya uchumi ili kufikia malengo ya kibinafsi ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.