Kenya: Shughuli za kibiashara zimeonekana kutatizika katika baadhi ya miji
Maafisa wa polisi wa kupambana na ghasia wameonekana katika maeneo tofauti ya mji mkuu wa Kenya kabla ya maandamano ya kuipinga kupanda kwa gharama ya maisha yaliopangwa na upinzani katika taifa hilo la Afrika Mashariki.
Imechapishwa:
Picha zilizochapishwa na vyombo vya habari vya ndani zimeonyesha vizuizi vya barabarani vikiwa vimewekwa katika maeneo tofauti ya jiji kuu Nairobi.
Shughuli za kibiashara katikati mwa jiji kuu zimeonekana kutatizika, maduka mengi tu yakiwa yamefungwa wakati baadhi ya magari ya uchukuzi wa umma yakionekana kuwa machache ikilinganishwa na siku nyengine.
Empty streets, closed businesses in Nairobi CBD ahead of anti-gov’t protests
— Citizen TV Kenya (@citizentvkenya) July 19, 2023
#MaandamanoWednesdayToFriday pic.twitter.com/fgAczoQkDt
Mjini Kisumu, barabara mbalimbali zimefungwa na waandamanaji ambao wameonekana wakiwa wamewasha moto magurudumu ya magari ,Maduka pia yamefungwa usafiri wa umma ukionekana kutatizika.
Maafisa wa polisi tayari wametumwa katika maeneo muhimu karibu na mji huo, upinzani ukisisitiza utaendelea na maadamano yake kama ilivyopangwa.
Hali sawa na hiyo pia imeshuhudiwa katika mji wa Migori ambapo shughuli za uchukuzi zimeathirika wakati biashara zikiwa zimefungwa, idadi kubwa ya maofisa wa polisi wakionekana wakipiga doria.
Maeneo ya Kitengela, kaunti ya Kajiado ambapo maandamano ya vurugu yalishuhudiwa wakati wa maandamano ya awali, maofisa wa polisi wametumwa huko pia, shughuli ndogo za kibiashara zikiendelea.
One person arrested as anti-government protests rock Mombasa #MaandamanoWednesdayToFriday pic.twitter.com/tyRZREq4um
— Citizen TV Kenya (@citizentvkenya) July 19, 2023
Katika maeneo mengine, polisi wamewakamata baadhi ya watu waliokuwa wamejitokeza kuaandamana.