Pata taarifa kuu

Kenya: Upinzani na serikali zatakiwa kutatua changamoto zao kwa amani

Nairobi – Wajumbe kutoka nchi za Marekani, Uingereza , Canada ,Ujerumani na mataifa mengine tisa wameeleza kuguswa na machafuko na vifo vilivyoripotiwa wakati wa maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha nchini Kenya.

Wito umetolewa kwa serikali nchini Kenya na upinzani kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani
Wito umetolewa kwa serikali nchini Kenya na upinzani kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Mabalozi hao kumi na watatu wametoa wito kwa pande husika katika mzozo huo kutatua changamoto zao kwa njia ya amani.

Wito huu unakuja wakati huu upinzani kupitia hotuba yake kwa vyombo vya habari nchini humo ukisisitiza kuendelea na maandamano yao ya siku tatu licha ya serikali kuonya kwamba hatafanyika.

Katika taarifa yao, mabalozi hao wamesema kwamba wanatambua changamoto zinazowakabili raia katika taifa hilo la Afrika Mashariki na kwamba wanatoa wito kwa serikali na upinzani kuweka matakwa yao wazi ilikupata suluhu ya kuendeleza nchi hiyo.

Serikali ya Nairobi imesisitiza kwamba haitaruhusu kufanyika kwa maandamano mengine yenye vurugu, upinzani ukisema wafuasi wake hawafanyi maandamano yenye vurugu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.