Kenya: Watu 300 wamekamatwa kwa kushiriki maandamano ya upinzani
Nairobi – Nchini Kenya, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema zaidi ya watu 300, ikiwa ni pamoja na mbunge mmoja wamekamatwa kufuatia maandamano ya kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha yaliyoharamishwa na polisi na kusababisha vifo vya watu saba na kuwaacha wengine nba majeraha.
Imechapishwa:
Baada ya maandamano hayo yaliyotishwa na upinzani na kugeuka kuwa ya vurugu kati ya waandamanaji na polisi, shughuli za kawaida zimeanza kurejelewa tena.
Hawa ni baadhi ya Wakenya waliorejelea majukumu yao baada ya maandamano ya jana.
“Mimi hufanya kazi ya kuweka magari vidhibiti mwendo lakini wakati wa maandamano hata sikwenda kazi hilo limeniumiza sana.” Walisema baadhi ya raia wa taifa hilo.
Baadhi ya raia wa Kenya waliorejelea majukumu yao
Watetezi wa haki za binadamu, wamewashtumu polisi kwa kutumia nguvu kupita kisiasa kukabiliana na waandamanaji.
Samson Omondi .ni kutoka Shirika la kutetea haki za binadamu nchini Kenya-KHRC.
“Kumekuwa na ukiukaji wa haki za binadamu kutokana na namna maofisa wa polisi walitumia nguvu wakati wa maandamano.” Samson Omondi, mtetezi wa haki za binadamu nchini kenya.
Samson Omondi, Mtetezi wa haki za binadamu nchini kenya
Naibu rais Rigathi Gachagua amemhstumu kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa maafa na uharibu uliofanyika.
“Huyu ndiye anatuletea shida nchini Kenya na matatizo yetu yataisha iwapo tutamalizana naye.”alisema naibu wa raisRigathi Gachagua.
Naibu rais Rigathi Gachagua
Odinga amesisitiza kuwa ataitisha maandamano zaidi katika siku zijazo, hadi pale rais William Ruto atakapokubali kupunguza gharama ya maisha miongoni mwa mambo mengine.