Pata taarifa kuu

Kenya: Sitaruhusu maandamano ya upinzani kufanyika: Rais Ruto

Nairobi – Rais wa Kenya William Ruto ameapa kutoruhusu kufanyika kwa maandamano ya upinzani ambayo yamepangwa kufanyika wiki ijayo, Ruto akisema kwamba atamkabili Odinga.

Rais Ruto ameapa kumkabili kiongozi wa upinzani Raila Odinga
Rais Ruto ameapa kumkabili kiongozi wa upinzani Raila Odinga AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika mji wa Naivasha katika eneo la bonde la ufa, rais Ruto amesema kwamba uchaguzi ulitamatika na hakuna mtu yeyote anayeweza kutafuta uongozi kwa kutumia damu ya wakenya na kuharibu mali.

Ruto amemtaka Odinga kusubiri hadi mwaka mwa 2027 wakati wa uchaguzi mkuu ujao na kwamba serikali haitaruhusu kufanyika kwa maandamano ya aina yoyote.

Aidha, mkuu huyo wa nchi amerejelea msimamo wake wa awali kwamba hatafanya mapatano yoyote ya kisiasa na upinzani na kwamba hatatingishwa na matakwa ya upinzani.

Matamshi ya mkuu wa nchi yamekuja muda mfupi baada ya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya wake Odinga kutangaza kurejelewa kwa maandamano kote  nchini humo kwa siku tatu kila wiki.

Katika taarifa yake, uongozi wa upinzani umeeleza kwamba maandano yajayo yatafanyika Jumatano, Alhamis na Ijuma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.