Pata taarifa kuu

Kenya: Mahakama imekataa kusitisha amri kuhusu utekelezwaji wa sheria ya fedha

Mahakama kuu nchini Kenya, Jumatatu ya juma hili ilitupilia mbali ombi la Serikali kutaka zuio la kutekelezwa kwa muswada tata wa kodi liondolewe, serikali ikisema sheria hiyo ni muhumu kutekelezwa ili iweze kulipa madeni yake kwa wakati na kutengeneza ajira.

Rais wa Kenya William Ruto na serikali yake wanasema sheria hiyo inalenga kukusanya mapato zaidi kulipa madeni ya taifa hilo
Rais wa Kenya William Ruto na serikali yake wanasema sheria hiyo inalenga kukusanya mapato zaidi kulipa madeni ya taifa hilo REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Jaji Mugure Thande, akitoa uamuzi wake ,amesema upande wa  malalamishi kwenye kesi hiyo akiwemo seneta wa Busia Okia Omtatah ,ulikuwa na msingi wa kutosha kutaka mahakama kuzuia utekelezwaji wa makataa ya sheria hiyo.

Ametaka  amri ya awali ya mahakama kusalia kwa juma lingine, ameamuru faili ya kesi hiyo kuwasilishwa kwa jaji mkuu Martha Koome ili kuunda kamati ya  majaji watatu kuskiliza kesi hiyo.

Ingawa jaji hakuweka bayana ,undani kuhusu kesi hiyo ,amesisitiza kuondoa marufuku hiyo itakuwa hatari kwa umma ambapo wanaweza kulazimika kuwa chini ya sheria inayokwenda kinyume cha katiba.

Mwanasheria mkuu nchini kupitia mawakili wake akiongozwa na mwanasheria mkuu wa zamani Githu Muigai, alikuwa amekataa rufaa ,kutaka amri hizo za mahakama kutupiliwa mbali.

Baadhi ya vipengee tata kwenye sheria hiyo ni ushuru wa asilimia 16 kwenye bidhaa za mafuta na ushuru wa nyumba ambao mfanyikazi na mwajiri wanachangia asilimia moja nukta tano.

Upinzani, umeitisha maandamano siku ya Jumatano, kushinikiza kuondolewa kwa sheria hiyo, iliyoongeza kodi iliyosababisha pia kupanda kwa bei ya mafuta.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amefisia uamuzi huo wa mahakama kukataa kuondoa marafuku ya utekelezwaji wa sheria hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.