Pata taarifa kuu

Kenya: Wanaharakati waliokuwa wamekusanyika nje ya kituo cha polisi wametawanywa

Nairobi – Maofisa wa polisi jijini Nairobi wamewatawanya watetezi wa haki za binadamu nchini humo waliokuwa wamefika katika kituo cha polisi cha Central wakitaka kuachiwa  kwa wenzio waliokamatwa wakati wa maandamano ya Ijumaa dhidi ya serikali.

Polisi hapo jana Ijumaa walikabiliana na waandamanaji waliokuwa wakipinga kupanda kwa gharama ya maisha
Polisi hapo jana Ijumaa walikabiliana na waandamanaji waliokuwa wakipinga kupanda kwa gharama ya maisha AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa picha na video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, wanaharakati hao wameonekana wakitwanya na walinda usalama kwa mabomu ya machozi wakati wengine wakikamatwa.

Jaji mkuu wa zamani wa Kenya Dkt Willy Mutunga ni miongoni mwa waandamanaji waliokuwa wamejitokeza kushinikiza polisi kuwachia wanaharakati hao wanaoshikiliwa katika kituo hicho.

Bonfence Mwangi, mwanaharakati mashuhuri nchini humo kupitia mitandao yake ya kijamii amewataka viongozi wa upinzani Raila Odinga na Martha Karua kushinikiza kuachiwa kwa watu hao ambao walikuwa miongoni mwa Wakenya waliojitokeza kuitikia wito wao wa kuandamana.

Maelfu ya raia katika taifa hilo la Afrika Mashariki waliandamana siku ya Ijumaa ya wiki hii katika maeneo mbalimbali kulalamikia kupanda kwa gharama ya maisha pamoja na ushuru unaongeza bei ya bidhaa za petroli.

Mtu mmoja amewauwa kwa kupigwa risasi huku wengine wengi wakiwa wamejeruhiwa ,wakati wa maandamano ya saba saba nchini Kenya ,yaliyoongozwa na kinara wa upinzani Raila Odinga ,kupinga gharama ya juu ya maisha.

Raila akizungumzwa wakati wa maandamano hayo ambayo msafara wake ulishambuliwa na maofisa wa polisi ,amesema matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola ,hayatamaliza juhudi za upinzani kutetea maslahi ya raia.

Muungano wa upinzani, wa Azimio la Umoja ,umesema kuwa maandamano hayo yataendelea jumatano wiki ijayo huku muungano huo ukiendelea na ukusanyaji wa saini milioni moja kufanikisha kura ya maoni ya kutaka kuondolewa wa utawala wa Kenya Kwanza wake rais Ruto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.