Pata taarifa kuu

Kenya: Idadi ya waliofariki katika maandamano imefikia watu wawili

Nairobi – Idadi ya watu waliouawa katika maandamano nchini Kenya imefikai watu wawili kwa mujibu wa taarifa kutoka katika hosipitali moja nchini humo, hatua inayokuja baada ya kinara wa upinzani kwenye taifa hilo Raila Odinga kuwataka raia kuandamana kupinga kuongezeka kwa ushuru.

Polisi wamekabiliana na wafuasi wa upinzani jijini Nairobi na maeneo mengine
Polisi wamekabiliana na wafuasi wa upinzani jijini Nairobi na maeneo mengine AP - Brian Inganga
Matangazo ya kibiashara

Siku siku ya Ijumaa waliwatawanya maelfu ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana na msafara wa Odinga jijini Nairobi hali sawa na hiyo ikishuhudia katika miji ya Mombasa na Kisumu.

"Tumesajili kifo kingine cha mtu mmoja na kufanya idadi ya vifo kufikia watu wawili kutokana na maandamano yaliofanyika jana," George Rae, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Jaramogi Oginga Odinga katika kaunti ya  Kisumu, ngome ya upinzani kwenye  eneo la Ziwa Victoria.

Haya yanajiri baada ya mapema leo Jumamosi, polisi kutumia mabomu ya  kutoa machozi kuwatawanya wawakilishi wa mashirika ya kiraia, akiwemo jaji mkuu wa zamani Willy Mutunga, ambao walikuwa wakitaka kuachiliwa kwa makumi ya watu waliokamatwa  wakati wa maandamano.

"Si haki hata kidogo kwa polisi kuturushia mabomu ya machozi wakati tumekuja kwa amani kutaka kuachiliwa kwa wanaharakati wasio na hatia waliozuiliwa katika seli tangu jana", alisema wakili Lempaa Suyianka.

"Baadhi yao walijeruhiwa na wanahitaji matibabu," aliwaambia wanahabari.

Msemaji wa Odinga Dennis Onyango aliambia AFP Jumamosi kwamba muungano wake wa Azimio unapanga kufanya “maandamano angalau siku moja ya kila wiki" dhidi ya sera za serikali ya Rais William Ruto, wakati maandamano mengine yakitarajiwa kufanyika Jumatano ya wiki ijayo.

Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani waliokuwa wakiandamana awali
Polisi walikabiliana na wafuasi wa upinzani waliokuwa wakiandamana awali REUTERS - MONICAH MWANGI

Wiki jana, Ruto alitia saini kuwa sheria mswada wa fedha unaotarajiwa kuipa serikali  zaidi ya dola bilioni 2.1 kwa hazina ya serikali inayokabiliwa na changamoto kama njia moja ya kupiga jeki uchumi wa taifa hilo.

Sheria ya fedha inatoa kodi mpya au ongezeko la bidhaa za kimsingi kama vile mafuta na chakula na uhamishaji wa pesa kwa njia ya simu, pamoja na ushuru wenye utata kwa walipa kodi wote ili kufadhili mpango wa nyumba. Serikali inasema ushuru huo utasaidia kuunda nafasi za kazi na kupunguza ukopaji wa umma.

Mahakama kuu ya Nairobi mwezi uliopita ilisitisha utekelezaji wa sheria hiyo baada ya seneta wa Busia Okiya Omutata kuwasilisha kesi kupinga uhalali wake wa kikatiba.

Lakini mdhibiti wa kawi nchini Kenya hata hivyo alitangaza kupanda kwa bei ya pampu baada ya kuongezeka maradufu kwa ushuru wa thamani hadi asilimia 16 kama ilivyoainishwa katika sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.