Pata taarifa kuu

Kenya: Odinga anaongoza wafuasi wake kupinga kupanda kwa gharama ya maisha

Nairobi – Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, ameongoza mkutano wa kisiasa katika uwanja wa kihistoria wa Kamkunji jijini Raila kupinga kile wanachosema ni kupanda kwa gharama ya maisha ambapo pia amewataka wafuasi wake kuandamana hadi katika jiji kuu.

Upinzani nchini Kenya unapinga sheria mpya iliyopitishwa na serikali kuhusu kodi
Upinzani nchini Kenya unapinga sheria mpya iliyopitishwa na serikali kuhusu kodi REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa polisi wameonekana katika miji mbalimbali ya taifa hilo kuwakabili waandamanaji waliojitokeza kuitikia wito wa kiongozi wa upinzani kuandamana kupinga sheria tata inyaopendekeza kupanda kwa ushuru wa bidhaa.

Katika kaunti ya Mombasa, pwani ya taifa hilo la Afrika Mashariki, polisi wametawanya kwa vitoa machozi waliokuwa wamekusanyika kwenye maeneo tofauti katika kaunti hiyo.

Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga na muungano wake wa  Azimio wamekuwa namkutano jijini Nairobi  kabla ya kuanza maandamano dhidi ya serikali kulalamikia sheria hiyo mpya wanayodaiwa inawaongezea mzigo raia ambayo tayari wanakabiliwa na changamoto za kimaisha.

"Rais William Ruto anatutoza ushuru bila idhini yetu na kutunga sheria ambazo matokeo yake ni kufanya maisha kuwa magumu," Azimio ilisema kwenye taarifa iliyotolewa mapema wiki hii.

Ruto wiki jana alitia saini kuwa sheria mswada wa fedha ambao unatarajiwa kusaidia serikali yake kupata zaidi ya dola bilioni 2.1 kwa hazina ya serikali iliyopungua na kusaidia kukarabati uchumi wa taifa hilo unaokabiliwa na madeni makubwa.

Tofauti na iliyokuwa kwa maandamano ya awali, wakati huu yameonekana kufanyika katika baadhi ya maeneo ya mishinani.

Sheria hiyo ya fedha imeongeza ushuru mpya au ongezeko la bidhaa mbalimbali za kimsingi kama vile mafuta na chakula na uhamishaji wa pesa kwa njia ya simu, pamoja na ushuru wenye utata kwa Wakenya wote wanaolipa ushuru kufadhili mpango wa makazi yenye bei nafuu.

Mahakama kuu jijini Nairobi Ijumaa iliyopita ilisitisha utekelezaji wa sheria hiyo baada ya seneta wa Busia, Magahribi ya taifa hilo Okiya Omutata kuwasilisha kesi kupinga uhalali wake wa kikatiba.

Licha ya uamuzi huo, bodi ya kudhibiti nishati nchini Kenya baadaye siku hiyo ilitangaza kupanda kwa bei ya mafuta ili kuzingatia kuongezeka kwa ushuru wa hadi asilimia 16 kama ilivyoainishwa katika sheria hiyo yenye utata.

Maandamano hayo yamepewa jina la "Saba Saba"  huku yakifanyika siku ya saba ya mwezi wa saba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.