Pata taarifa kuu

Kenya: Polisi wakabiliana na wafusi wa upinzani jijini Nairobi

Nairobi – Polisi jijini Nairobi wameushambulia msafara wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga kwa mabomu ya machozi  baada ya kuhutubia mkutano mkubwa katika uwanja wa kishtoria wa Kamkunji jijini Nairobi, polisi wakichukua hatua sawa na hiyo ya kuvunja maandamano katika mji Mombasa na Kisumu.

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga © Raila Odinga
Matangazo ya kibiashara

Polisi walikuwa wametumwa kuzuia maandamano ya hivi punde zaidi yaliyoitishwa na Odinga mwaka huu kuhusu sera za serikali ya Rais William Ruto.

Katika mkutano huo, Odinga ambaye alishindwa katika uchaguzi wa Agosti 2022 na  Ruto  alitangaza mipango ya kukusanya saini milioni 10 katika jitihada za kumwondoa mpinzani wake mkuu madarakani.

"Wakenya walichagua viongozi bungeni na wamewasaliti," alisema huku akishangiliwa. "Ruto mwenyewe ambaye alichukua mamlaka kinyume cha sheria amewasaliti Wakenya." alisema Odinga.

Muungano wa Azimio wa Odinga ulikuwa umeitisha maandamano kuhusu athari za ushuru huo mpya kwa Wakenya ambao tayari wanakabiliwa na matatizo ya kiuchumi na kupanda kwa bei ya mahitaji ya kimsingi.

Wiki jana, Ruto alitia saini kuwa sheria mswada wa fedha ambao unatarajiwa kuipa serikali  zaidi ya dola bilioni 2.1 kwa hazina ya serikali inayokabiliwa na changamoto na kusaidia kuimarisha uchumi wake  uliokumbwa na madeni makubwa.

Sheria ya fedha inatoa ushuru mpya au ongezeko la bidhaa mbalimbali za kimsingi kama vile mafuta na chakula na uhamishaji wa pesa kwa njia ya simu, pamoja na ushuru wenye utata kwa Wakenya wote wanaolipa ushuru kufadhili mpango wa makazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.