Pata taarifa kuu
Kenya - Usalama

Kenya : Kuwekeza katika walinzi wa binafsi

Kenya – Serikali Kenya inalenga kutoa mafunzo ya kuimarisha ujuzi wa  matumizi ya vifaa vya hali ya juu vya ulinzi kwa wakenya zaidi ya 900, 000 walioajiriwa katika sekta ya kutoa ulinzi wa binafsi, baada ya kuzinduliwa kwa taasisi ya kwanza ya mafunzo ya usalama wa kibinafsi mjini Eldoret.

Walinzi wa binafsi nchini Kenya
Walinzi wa binafsi nchini Kenya © Wizara ya mambo ya ndani Kenya
Matangazo ya kibiashara

 

Katibu wa mambo ya ndani wa Kenya, Raymond Omollo kushoto akitoa cheti kwa mlinzi wa binafsi.
Katibu wa mambo ya ndani wa Kenya, Raymond Omollo kushoto akitoa cheti kwa mlinzi wa binafsi. © Wizara ya mambo ya ndani Kenya

Katibu katika wizara ya mambo ya ndani Raymond Omolo, amesema serikali ya Kenya tayari imeanza mchakato wa kutoa nambari za kikosi cha ulinzi kwa walinzi binafsi ambao watakuwa kwenye mafunzo ili kuwawezesha kukabiliana  na tishio la usalama ambalo kwa sasa limeongezeka nchini Kenya, kutokana na mashambulizi kutoka kwa kundi la kigaidi la Al Shabaab.

Aidha Raymond ameongeza kuwa serikali ya Kenya itatoa zana za kinga na magari ya ya kiufundi kwa walinzi binafsi katika mwaka huu wa kifedha 2023/24.

 

Walinzi wa binafsi nchini Kenya
Walinzi wa binafsi nchini Kenya © Wizara ya mambo ya ndani Kenya

 

Uzidunzi wa taasisi hiyo ya  mafunzo ya usalama kwa jina Miale, imedhamiria kubadilisha sekta ya usalama kupitia mitaala na miongozo ya mafunzo ya usalama.

Haya yanajiri wakati huu serikali ya Kenya, imelazimika kusitisha mpango wake wa kufungua mipaka ya ardhini na taifa jirani la Somalia, kufutia ongezeko la mashambulizi kutoka kwa watu wanaodhaniwa kuwa wanajihadi wa Al Shabaab, ambao kwa kipindi cha miezi mitatu wamewaua zaidi ya watu 30 wakiwemo maafisa wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.