Pata taarifa kuu
KILIMO-UCHUNGUZI

Tanzania: Bakteria waathiri mazao ya mpunga

Nchini Tanzania, kuna ugonjwa unaoharibu mazao ya mpunga. Janga ambalo linashika kasi: karibu 20% ya mashamba ya mpunga nchini yameathirika, kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania. Hii inaweza kuwa ilisababishwa na majaribio ya mbegu yaliyofanywa wakati wa ushirikiano kati ya watafiti wa kilimo wa China na Tanzania.

Shamba la mpunga nchini Tanzania katika wilaya ya Itigi mnamo 2020.
Shamba la mpunga nchini Tanzania katika wilaya ya Itigi mnamo 2020. © Wikimedia Commons CC BY SA 4.0 Charstone Simon
Matangazo ya kibiashara

Wengine tayari wanauita ugonjwa huo "Uviko" wa mchele. Bakteria hii ya Xoo (Xanthomonas oryzae pathovar oryzae) huingia kwenye majani, hushambulia mmea na kuukausha. Hivyo, nafaka ya mchele inakosa ujazo, hali ambayo ina athari za mavuno.

Sehemu ya tano ya uzalishaji itaathiriwa kulingana na wataalam kadhaa wa Kitanzania waliohojiwa. "Wazalishaji tuliokutana nao mashambani walituambia kwamba mwaka jana walivuna magunia ya mchele mara mbili kwa kila shamba ikilinganishwa na mwaka huu," anaelezea Boris Szurek, mtaalamu wa magonjwa ya mimea katika IRD, Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo nchini Ufaransa ambaye amerejea kutoka nchini Tanzania kufuatili janga hili. Miaka kumi iliyopita tulipokuja katika ardhi hiyo, hakukuwa na chochote kuhusu ugonjwa huu wa bakteria. Walakini, mwaka huu, kuna mlipuko wa janga hilo, ni hali ambayo inatia wasiwasi sana ”.

Mbegu zinazoambukiza ugonjwa huo?

Uchomaji huu wa bakteria ulionekana Morogoro, mkoa unaolima mpunga, lakini pia katika mikoa ya Muenza na Arusha. Hata hivyo wanasayansi wameona ugonjwa huo karibu na Mombasa nchini Kenya. Ugonjwa huo unaenea, na unaathiri sehemu kubwa sana ya mashamba, kwa mujibu wa Ibrahim Hashim wa taasisi ya utafiti wa kilimo nchini Tanzania: "Katika maeneo yote ambayo kuna umwagiliaji, nusu ya mashamba yameathirika. Changamoto iliyopo ni kusambaza katika mikoa hii mbegu zenye afya, kwa sababu hofu yangu ni kwamba iwapo wakulima wataendelea kupata mbegu zinazobeba bakteria hao tatizo litaendelea kwa muda mrefu sana”.

Uchunguzi unaendelea kupata chanzo cha janga hili, inasema mamlaka. Mbegu hizo zinaweza kuwa vekta za bakteria, ambazo zinaweza kuelezea usambazaji kwa umbali huo mkubwa. Utafiti unafanywa hasa katika IRD. Tunachojua kwa hakika: kuungua kwa kwanza kwa mimea ya mpunga kulionekana mwaka wa 2019 karibu na Dakawa mkoani Morogoro. Hapa ndipo pia kilipo kituo cha utafiti cha Tanzania - Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) - ambayo ilianza ushirikiano wa karibu na China karibu miaka 10 iliyopita.

Vipimo na tafiti mbalimbali kuhusu mbegu zinazotoa mavuno mengi hufanyika. Hata hivyo, ni aina ya bakteria wa bara la Asia ambao wanapatikana Tanzania, hawakuwahi kuonekana Afrika Mashariki hapo awali, hivyo basi nadharia hii ilitengenezwa na timu ya watafiti wa kimataifa akiwemo Boris Szurek kutoka 'IRD: "Nadhani ni wazi kuwa ni bahati mbaya, lakini kwa mujibu wa uchambuzi wetu, bila shaka wameingiza bakteria wanaotoka jimbo la Yunnan, na ambao sasa wanasambaa nchini, anaeleza mtafiti huyo, tunafahamu kuwa Wachina wameingiza mbegu za mpunga zisizo faa kwa kuzipanda kwenye shamba la majaribio ili kuonyesha umma, wafugaji wa ndani na wakulima kwamba aina zao zimefanikiwa na zinatoa mazao mengi. Shida ni kwamba pia wameanzisha kijidudu hiki ambacho ni bomu la wakati kwa Afrika Mashariki”.

Wasiwasi wa usalama wa chakula nchini

Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa mpunga katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Inaagiza kiasi kidogo kutoka Pakistani, na kutengeneza baadhi ya bidhaa nje, hasa katika Afrika Mashariki. Nchi inakaribia kujitegemea, lakini kutokana na mavuno kidogo kwa asilimia 20, "inaweza kujikuta katika hali ngumu, na hatimaye kuwa tegemezi kwa soko la nje", kulingana na mwanauchumi aliyebobea katika sekta ya mpunga.

Bei ya mchele wa kienyeji tayari imeongezeka na hali inatia wasiwasi. "Linaweza kuwa tatizo kubwa kwa usalama wa chakula hapa," amesema Jason Jonathan Kanan, mshauri katika Kitivo cha Kilimo na Maliasili cha Dar Es Salaam. Tanzania inategemea uzalishaji wa mpunga, ni zao la pili nchini baada ya mahindi. Serikali inajaribu kudhibiti janga hili. Ugavi lazima uwe salama”

Suluhu zipo. Muungano wa kimataifa wa utafiti wa "Mazao Yenye Afya" unaoongozwa na Profesa Wolf B. Frommer wa Chuo Kikuu cha Heinrich-Heine cha Düsseldorf (HHU) unakuza aina za mpunga zinazostahimili magonjwa. Kulingana na Boris Szurek, itakuwa muhimu "kuanzisha jeni sugu katika aina za mpunga zinazopatikana Tanzania ili kukabiliana na aina hizi za bakteria". Utafiti wa muda mrefu wa kumaliza janga ambalo linahangaisha mamlaka ya Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.