Pata taarifa kuu

Kenya : Upinzani kurejelea maandamano kupinga kupandishwa kwa kodi

Nairobi – Muungano wa upinzani nchini Kenya, wa Azimio umewataka wafuasi wake kususa ulipaji ushuru kama njia moja ya kupinga kile muungano huo umetaja kama ukandamizaji wa serikali ya Rais William Ruto.

Upinzani nchini Kenya unapinga sheria mpya iliyopitishwa na serikali kuhusu kodi
Upinzani nchini Kenya unapinga sheria mpya iliyopitishwa na serikali kuhusu kodi REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano wao wa hadhara hapo jana, kiongozi wa upinzani Raila Odinga, amewataka waajiri pia kuunga mkono juhudi za kushinikiza kufutwa kwa sheria ya fedha.

Hatuwezi kutishwa na watu wachache ambao waliiba kura zetu, tunafahamu namna walivyotuibia, tunawaeleza kwamba wakenya wanataka hivi nao hawaelewi. alisema Odinga.

00:26

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga

Aidha Odinga ametangaza kuwa maandamano ya kitaifa yatarejeshwa ili kuishinikiza serikali kufuta kwa sheria ya fedha iliosainiwa na rais Ruto mapema wiki hii.

Haya yanajiri siku chache baada ya Rais Ruto kutia saini hatua hizo tata za ushuru kuwa sheria baada ya kupitishwa na wabunge wiki jana.

Sheria hiyo mpya inapandisha ushuru wa ongezeko la thamani kwa bidhaa za mafuta kutoka asimilia 8 hadi asimilia 16.

Raia katika taifa hilo la Afrika Mashariki pia wanatarajiwa kuaanza kukatwa tozo ya nyumba ya asilimia 1.5 kwa malipo ya msingi ya wafanyikazi, ambayo itatozwa kwa mwajiri na mwajiriwa. Pesa hizo zinatakiwa kwenda kwenye mfuko wa kujenga nyumba za watu wenye maisha duni.

Upinzani umesema utarejelea maandamano baada ya serikali kuidhinisha sheria hiyo
Upinzani umesema utarejelea maandamano baada ya serikali kuidhinisha sheria hiyo REUTERS - THOMAS MUKOYA

Rais Ruto ametetea sheria hiyo mpya akisema kuwa hazina ya nyumba inalenga kujenga nyumba za bei nafuu kwa watu wa kipato cha chini na kuzalisha nafasi za kazi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.