Pata taarifa kuu

Visa vya Kipindupindu katika kaunti ya Homabay Magharibi ya Kenya vyaongezeka

NAIROBI – Nchini Kenya, mwezi uliopita Wizara ya afya, ilitoa tahadhari ya mlipuko wa kipindupindu katika Kaunti za Siaya na Homabay, Magharibi mwa nchi hiyo baada ya kuripotiwa kwa maambukizo na vifo.Mwandishi wetu George Ajowi ambaye alikuwa ziarani huko Homabay, amethathmini hali halisi kuhusu mlipuko huu na kutuandalia ripoti ifuatayo……

Mji wa Homabay Magharibi ya Kenya, ni mojawapo ya maeneo maarufu kwa uvuvi wa samaki
Mji wa Homabay Magharibi ya Kenya, ni mojawapo ya maeneo maarufu kwa uvuvi wa samaki © AFP/Simon Maina
Matangazo ya kibiashara

Soko ya Sindo katika eneo la suba Mashariki kaunti ya homabay limeanza kupata uhai wiki chache tu baada ya kufungwa baada ya mlipuko wa Kipindupindu.

Kufungwa kwa soko hili, baada ya watu kadhaa kuambukizwa, kumeathiri hali ya biashara. Jane Okech ni mafanyabiashara wa mgahawa.

“Tangu kuaanza kwa hii hali ya kipindupindu, wateja wamepungua kwa kiasi kikubwa. “alisema Jane Okech, mafanyabiashara wa mgahawa.

00:03

Jane Okech, mafanyabiashara wa mgahawa

Soko hili ambalo wanunuzi na wauzaji zaidi ya Elfu mbili, huja kila siku, lina choo kimoja tu.

“Tunateseka sana hii choo hapa imejaa.” alisema mmoja wa wafanyibiashara katika soko hili.

00:02

Mfanyibiashara katika soko hili

Baada ya kuzuka kwa ugonjwa huo, baadhi ya wakaazi na watu wanaokuja kwenye soko hili, sasa wameanza kupata elimu ya kuuzuia. Moses Odhiambo ni mchuuzi.

“Hoteli zote zilifungwa sasa maofisa katika idara ya afya wameweka sheria kwamba iwapo hauna barua hakuna kufungua hotel. ” alisema Moses Odhiambo,  mchuuzi katika soko hili.

00:06

Moses Odhiambo, mchuuzi

Mwezi Machi mwaka huu, mlipuko wa ugonjwa huu uliripotiwa katika mataifa 13 ya Afrika kama vile Burundi, Kenya, Ethiopia, Msumbiji na Tanzania.

WHO imelaumu ongezeko la maambukizi ya ugonjwa huu duniani kutokana na umasikini, migogoro na mabadiliko ya tabia nchi.

George Ajwoi- RFI Kiswahili- Homabay

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.