Pata taarifa kuu

Uganda: Mazishi ya waliouawa katika shambulio la ADF yaanza kufanyika

NAIROBI – Mazishi za baadhi ya watu 42 wengi wao wanafunzi wa Shule ya Sekondari waliouawa baada ya kushambuliwa na waasi wa ADF mwishoni mwa wiki iliyopita katika mji wa Mpondwe, nchini Uganda karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, yameanza kufanyika, huku wakaazi wa eneo hilo, wakihofia usalama wao.

Baadhi ya familia zimeanza kuwazika wapendwa wao
Baadhi ya familia zimeanza kuwazika wapendwa wao AP - Hajarah Nalwadda
Matangazo ya kibiashara

Onesimus Kingwana alipoteza watoto wawili wa kiume katika shambulio hilo. Mmoja alikuwa mlinzi katika shule na mwingine alikuwa mwanafunzi katika hilo shule.

Istoshe mjukuu wake wa kiume ni miongoni mwa wale waliochukuliwa na waasi wa ADF.

“Sio mbali sana na eneo la tukio japokuwa hakuna aliyejitokeza kusaidia.” alisema Onesimus Kingwana, aliyepoteza wapendwa wake katika shambulio hilo.

00:14

Onesimus Kingwana, raia wa Uganda

Mary Masika, jirani wa karibu wa shule bado ana kiwewe huku Loyce Biira jirani mwingine akitafakari kuondoka katika kijiji.

“Mimi sikulala hapa, maana nina hofu akilini mwangu kuwa huenda hawa wavamizi wakarudhi tena.” alieleza mmoja wa raia wanaoishi jirani na shule hiyo.

00:20

Raia wa Uganda, jirani na kulikotokea shambulio

Vikosi vya usalama vinasema kuwa hali ni shwari na tayari watu 20 wanaoshukiwa kuwa washirika wa waasi wa ADF wamekamatwa. 

Godfrey Kabbyanga ni naibu waziri katika wizara ya habari nchini Uganda.

“Ulinzi upo, UPDF imeongeza nguvu, watu wasiwe na wasiwasi hakuna tatizo kabisa.” alithibitisha Godfrey Kabbyanga

00:07

Godfrey Kabbyanga, Naibu waziri katika wizara ya Habari

Baadhi ya familia zilizopoteza jamaa zao zimewazika lakini wapo wanaosubiri usaidizi wa kisayansi kutambua kikamilifu miili iliyoungua kwa kiasi. Jamii zingine zinasubiri habari kuhusu watoto wao waliotekwa nyara na waasi.

Kenneth Lukwago, Kampala, RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.