Pata taarifa kuu

Watu wenye silaha wamewaua maofisa wawili wa usalama pwani ya Kenya

NAIROBI – Karibia wanajeshi wawili wa Kenya wameripotiwa kuawawa Jumapili ya wikendi iliyopita wakati maofisa wengine wa usalama 20 wakithibitishwa kujeruhiwa katika mashambulio yaliotekelezwa katika kaunti ya Lamu pwani ya taifa hilo la Afrika Mashariki mpaka na nchi ya Somalia.

 Al-Shabaab wanahusishwa na kundi Al-Qaeda
Al-Shabaab wanahusishwa na kundi Al-Qaeda AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Maofisa hao wa jeshi waliuawa katika shambulio la kushtukiza wakati wakienda kuwasaidia wenzao wa kitengo cha GSU ambao wanasaidiaina nao katika uimarishaji wa usalama kwenye eneo hilo ambao walikuwa wameshambuliwa.

Kwa mujibu wa taarifa, gari walimokuwa wakisafiria maofisa hao wa kitengo cha GSU, lilikanyaga kilipuzi kilichokuwa kimetegewa ardhini ambapo 12 kati yao walijeruhiwa.

Kumekuwa na ongezeko la mashambulio yanayotekelezwa na  watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabab huko Lamu katika wiki za hivi majuzi.

Watu wenye silaha waliwaua takriban maafisa 16 wa usalama tarehe 13 Juni huko Lamu na kaunti jirani ya Garissa.

Al-Shabab mara nyingi hufanya mashambulio mabaya katika eneo la  pwani ya kaskazini mwa Kenya na kaskazini-mashariki, wakidai kuwa wanalipiza kisasi kwa hatua ya  Nairobi kuwatuma  wanajeshi wake nchini Somalia mwaka 2011 kupambana na kundi hilo.

Serikali ya Kenya imekuwa ikiimarisha vita dhidi ya makundi ya kigaidi nchini humo haswa katika maeneo jirani na nchi ya Somalia ambapo wapiganaji wa al-Shabab wamekuwa wakitekeleza mashabulio dhidi ya raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.