Pata taarifa kuu

Idadi yawaliouawa katika shambulio la ADF nchini Uganda mpaka na DRC imefikia 40

NAIROBI – Idadi ya watu waliofariki katika shambulio la  katika  shule katika mmoja katika  mji wa Mpondwe magharibi mwa Uganda imeongezeka na kufikia 40 wakati huu idadi watu waliotekewa ikiwa haijulikani kulingana na meya wa mji huo na ripoti za vyombo vya habari vya ndani.

Zaidi ya watu 40 wamethibitishwa kufariki katika shambulio hilo karibu na DRC
Zaidi ya watu 40 wamethibitishwa kufariki katika shambulio hilo karibu na DRC © FMM
Matangazo ya kibiashara

Waliouawa ni pamoja na wanafunzi, mlinzi mmoja na watu wawili wa jamii ya eneo hilo ambao waliuawa nje ya shule hiyo, Meya wa Mpondwe-Lhubiriha Selevest Mapoze amethibitisha.

Kwa mujibu wa Mapoze, baadhi ya wanafunzi hao wanauuguza majeraha mabaya baada ya waasi hao kuteketeza bweni, wengine walipigwa risasi au kukatwakatwa na mapanga.

Hapo awali polisi walisema walikuwa wakiwafuatilia washambuliaji hao waliokimbia kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Virunga nchini DRC.

Joe Walusimbi, afisa anayemwakilisha Rais wa Uganda Yoweri Museveni huko Kasese, aliliambia shirika la habari la Associated Press kwa njia ya simu kwamba mamlaka inajaribu kuthibitisha idadi ya wahasiriwa na wale waliotekwa nyara."Baadhi ya miili ilichomwa kiasi cha kutoweza kutambulika," alisema.

Kundi la ADF linashutumiwa kwa kuanzisha mashambulizi mengi dhidi ya raia katika miaka ya hivi karibuni, hususan katika jamii za kiraia, katika maeneo ya mbali ya mashariki mwa DR Congo. Mwezi Aprili, kundi hilo lililaumiwa kwa shambulizi mashariki mwa DRC ambalo lilisababisha vifo vya takriban watu 20.

Mamlaka ya Uganda kwa miaka mingi imeapa kuwasaka wapiganaji wa ADF "ndani na nje ya nchi."

Kundi hilo linaaminika kuhusika na mauaji ya watu 36 mwezi Machi wakati wa shambulio la usiku katika kijiji cha Mukondi, mashariki mwa DRC.

Mamlaka ya Uganda pia ililaumu kundi hilo kwa mashambulio mabaya ya kujitoa mhanga katika mji mkuu, Kampala, mwaka 2021.

Wanajeshi wa Uganda UPDF wamekuwa wakiwasaka waasi wa ADF wanaominika kutorokea nchini DRC
Wanajeshi wa Uganda UPDF wamekuwa wakiwasaka waasi wa ADF wanaominika kutorokea nchini DRC © SEBASTIEN KITSA MUSAYI/AFP

Mnamo 2021, Uganda ilianzisha mashambulio ya pamoja ya anga na mizinga nchini DR Congo dhidi ya ADF.

Kundi la ADF, ambalo Marekani imeliona kuwa la "kigaidi", linachukuliwa kuwa la mauaji zaidi kati ya makumi ya wanamgambo wenye silaha ambao wanazurura kwa utajiri wa madini mashariki mwa DRC.

Mnamo 1995, ADF iliundwa na muungano wa vikosi vya waasi - ikiwa ni pamoja na Uganda Muslim Liberation Army na National Army for the Liberation of Uganda (NALU) - kupigana dhidi ya utawala wa Museveni.

Kwa miaka mingi, ADF iliungwa mkono na serikali zilizofuata za DRC ambazo zilikuwa na nia ya kupindua ushawishi wa Rwanda na Uganda nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.