Pata taarifa kuu

Uchafuzi wa mazingira unavyochangia uhaba wa samaki Ziwa Victoria

NAIROBI – Watalaam wa mazingira wanaonya kuwa uchafuzi wa mazingira katika ufuo wa Ziwa Victoria unaendelea kusababisha uhaba wa samaki katika Ziwa hilo linalotegemea na sehemu ya raia wa Magharibi ya Kenya.

Baadhi ya shughuli za kibinadamu zimetajwa kuchangia katika uchafuzi wa mazingira Ziwa Victoria
Baadhi ya shughuli za kibinadamu zimetajwa kuchangia katika uchafuzi wa mazingira Ziwa Victoria sarahemcc/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti ya mwisho kuhusu kinachosababisa upungufu wa samaki, wakaazi wa Miuru Bay katika Kaunti ya Migori wanatumia maji ya Ziwa kwa kuoga, kuosha vyombo na kutupa taka na kemikali nyingine bila kufahamu madhara yake.

Hali imetajwa kuathiri viumbe wa majini ama uchafuzi wa mazingira kwenye ziwa. Night Rose, ni mvuvi, anaeleza namna uchafuzi huu umeathiri samaki.  

“Nimeona wale samaki wadogo wadogo hawapo tena baharini.” alisema Night Rose, mvuvi.

00:24

Night Rose, mvuvi

Peter Odera Mtaalam wa mazingira anatoa sababu za samaki kupungua katika Ziwa ni kutokana na hatua ya baadhi ya raia wanaoishi jirani na Ziwa kumwaga maji machafu ziwani.

“Nikiongea kuhusu wale kina mama wanaosha vyombo inaathiri viumbe wa majini. “alisema Peter Odera Mtaalam wa mazingira.

01:08

Peter Odera Mtaalam wa mazingira

Ziwa Victoria ni mojawapo ya maziwa safi, lakini kwa wakaazi wanaoishi eneo hili, wanakabiliwa na  ugumu wa kujikumu kutokana na mabadiliko ya tabia nchini. Evans Otieno ambaye pia ni mvuvi, anapendekeza mbinu mbadala. 

“Serikali ituletee vifaa maalum vya kuhifadhi samaki kama vile nchi zengine zinavofanya.” alisema Evans Otieno, mvuvi.

00:32

Evans Otieno, mvuvi

Watalaam wanaonya kuwa iwapo uchafuzi wa Ziwa utaendelea, uhai wa samaki upo hatarini na miaka michache ijayo, wavuvi watakosa cha kuvua iwapo suluhu haitapatikana.

George Ajowi- RFI-Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.