Pata taarifa kuu

Mataifa ya EAC yasoma bajeti huku raia wakilalamikia gharama ya juu ya maisha

NAIROBI – Mawaziri wa fedha kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wamewasilisha makadirio ya fedha ya bajeti ya mwaka 2023/24 wakati raia wa nchi hizo wakilalamikia kupanda kwa gharama ya bidhaa muhimu hasa vyakula.  

(Katikati) Waziri wa fedha wa Kenya Prof. Njuguna Ndung’u, wakati wa kuwasilisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2023/2024 jijini Nairobi, Juni 15, 2023.
(Katikati) Waziri wa fedha wa Kenya Prof. Njuguna Ndung’u, wakati wa kuwasilisha makadirio ya bajeti ya mwaka 2023/2024 jijini Nairobi, Juni 15, 2023. © @KeTreasury
Matangazo ya kibiashara

Nchini Kenya, waziri wa fedha Njuguna Ndung'u, amewasilisha bajeti ya Shilingi trilioni 3.6, ikiwa ni kwanza ya utawala wa rais William Ruto, ambapo sekta ya elimu imepewa kipau mbele kwa kutengewa Bilioni 630.

Waziri Ndung'u amekadiria ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao.  

Uchumi unatarajiwa kuimarika kwa asilimia 5.5 mwaka huu kutoka asilimia 4.8 mwaka 2022, ukuaji utaimarishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali chini ya ajenda ya kiuchumi ya Bottom Up inayojumuisha utoaji wa mbolea ya ruzuku na mbegu kwa wakulima wakati wa msimu wa kupanda. Amesema Ndung'u.

00:23

Njuguna Ndung'u, waziri wa fedha nchini Kenya, Juni 15

Wakati akiwasilisha bajeti ya trilioni 44.38, waziri wa fedha na mipango  nchini Tanzania, Mwigulu Nchemba, ameelezea sababu za deni la taifa kuongezeka hadi Trilioni 79.  

 

Ongezeko la deni limetokana na kuwepo kwa fedha za mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli viwanja vywa ndege.... 

00:28

Mwigulu Nchemba, waziri wa fedha wa Tanzania, Juni 15

Nchini Uganda, licha ya changamoto za kiuchumi, waziri wa fedha Matia kasaija, amesema wanakadiria uchumi wa nchi hiyo kukuwa kwa asilimia 6 katika mwaka wa fedha wa 2023/2024.  

 

Mandhari ya bajeti yamebakia kuwa uchumaji kamili wa uchumi wa Uganda, kupitia kilimo cha biashara, viwanda, kupanua huduma, mabadiliko ya kidijitali na upatikanaji wa soko. Amesema Kasaija

00:13

Matia Kasaija, waziri wa fedha wa Uganda, Juni 15

Kule nchini Rwanda, serikali inapanga kutenga Franca za Rwanda trilioni 5 kwa maendeleo mbalimbali ya nchi hiyo.

Huko Burundi Waziri wa fedha Audace Niyonzima, amesema matumizi ya serikali yanatarajiwa kuongezeka hadi franca  trilioni 3.95 kutoka trilioni 2.39  mwaka uliopita.  

Bajeti za Jumuiya ya Afrika Mashariki husomwa kwa siku moja, na uwasilishaji wa mwaka huu unekuja wakati raia wa nchi hizo wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.